AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kubadilika kwa kujikurubisha mbele ya Mwenyezi Mungu (S.W) ili kupata radhi zake katika kulitumikia taifa kwa haki na uadilifu.

alternative

Al hajj Dk. Mwinyi, ametoa nasaha hizo aliposhiriki kwenye Kongamano la kiimani kwa viongozi na watendaji wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil, Kikwajuni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Al hajj Dk. Mwinyi alieleza, maratajio yake baada ya kongamano hilo ni kuona mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwa watumishi na wateule aliowapa majukumu ya kumsaidi kwenye utendaji na weledi wa kufanyakazi za kuwatumikia watu. “Ni matarajio yangu tutatoka na kitu tofauti hapa mara baada ya kongamano hili kwani limemgusa kila mmoja wetu, kazi iliopo mbele ni muhimu kujitathmini na kurekebisha mapungufu yaliopo.” alisihi Al hajj Dk. Mwinyi.

Akizungumza masuala ya utawala bora, nidhamu na maadili kwenye utumishi wa umma alieleza, ni msingi imara wa kutengeneza badala ya kulete maafa kwa kukosekana vyote hivyo. Dk. Mwinyi alilaumu ukiukwaji wa nidhamu ya utumishi wa umma unaofanywa na baadhi ya viongozi pamoja na kusifu nidhamu iliyopo kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo aliwasihi viongozi na watumishi wa Serikali kujenga uaminifu, maadili na kutenda haki kwa hofu ya kumuogopa Mwenyezi Mungu.

Akizungumzia masuala ya usimamizi wa Kodi, Al hajj Dk. Mwinyi alisisitiza haja ya kuzisimamia kwa haki na uadilifu wa hali ya juu sio kudhulumu watu. Alisema, kodi ni muhimu kwenye kufanikisha huduma bora za jamii na kueleza umuhimu wake umetajwa kwa kina kwenye hata kwenye vitabu vitukufu vya dini.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman alisifu kongamano hilo kuwa ni darasa lililowafunza viongozi wengi na kuwakumbusha kwenye wajibu wao wanaopaswa kutumikia umma kwa uadilifu kila
siku. Akizungumza kwenye Kongamano hilo, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandis Zena Ahmedi Saidi aliwataka watumishi wa umma kuwa Sehemu ya mabadiliko makubwa ya utendaji Serikali na kuwatumikia watu.

Mhandisi Zena pia aligusia suala la uadilifu na kueleza kuwa halipo kwenye vipimo vya bidhaa pekee hata kwenye utedaji na utumishi wa Umma akiwazungumzia watumishi wanaochakata masaa ya utumishi kwa kutoyakamiisha kwa uadilifu ni ukosefu wa
uadilifu na upungufu wa imani ya dhati mbele ya Mola (S.W). Hivyo, aliwaeleza viongozi za Serikali na watumishi wa umma kujitafakari na kujitathmini wanapovunja uaminifu kwenye utendaji wao sambamba na kuwaeleza kuwa wanabeba dhima kubwa kwa Mwenyezi Mungu kwa kutokuwa waadilifu kwenye kazi zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kongamano hilo lililokuwa na mnasaba na imaani za dini, Masheikh tofauti kutoka Tanzania na Mombasa, Kenya wakiwemo Sheikh Muhamad Al Hajir na Sheikh Izudin Alwy kutoka Kenya, Sheikh Nurdin Kishki
wa Dar es Salaam, Sheikh Shaaban Batash kutoka kamati ya Baraza la Maulamaa na Sheikh Khamis kutoka Kitengo cha Fatwa Ofisi ya Mufti, Zanzibar, waligusia masuala mbalimbali ya utumishi Serikalini ikiwemo nidhamu, ubinaadam kwenye uongozi,
utendaji, dhamana za vyeo, rushwa, uwajibikaji, uadilifu, kutunza siri na rasilimali za umma kwa mujibu wa nyadhifa wanazozitumikia, upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano, kujiepusha na hasadi na tamaa ni msingi ya uongozi bora kwenye utumishi
wa umma.

Kongamano hilo la kiimani kwa viongozi na watendaji wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilitayarishwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na kuratibiwa na Ofisi ya Mufti, Zanzibar lilikudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu