AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi amewataka wananchi kuzienzi na kuziendeleza  fikra na falsafa za kimaendeleo na kizalendo za Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume kwa maslahi ya Taifa.

alternative

Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika Kongmano la Sita (6) la kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume lililofanyika  katika Chuo cha Kumbukumbu ya mwalimu Nyerere Kampasi ya Karume Zanzibar.

Amesema kuwa Marehemu Mzee Karume alijenga upendo na umoja wa Kitaifa, misingi bora ya kiuchumi, kuleta haki na kupambana na dhuluma dhidi ya wanyonge, hivyo tunapaswa kumuenzi kivitendo kama ambavyo tunayathamini Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Dkt Mwinyi amefahamisha kuwa kutimia kwa miaka 52 ya kumbukizi ya Mzee Karume ni vyema kujikumbusha misingi ya utendaji wenye kuacha alama katika maisha na mifumo mbali mbali katika Serikali kwa kuendeleza na kukuza uzalendo miongoni mwetu.

Aidha Rais Dkt Mwinyi amesema kupitia Kongamano hili ni vyeme  jamii kukumbuka na kurejea katika misingi ya falsafa za uwazi, uadilifu, ushirikishwaji, amani, upendo na ubunifu na utendaji wenye kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, , Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe HAMZA HASSAN JUMA amesema Chuo cha Kumbukumbu ya Mwaliu Nyerere kinamuenzi kwa vitendo Hayati Mzee Karume kwa kuamua kila mwaka kufanya Kongamano ambalo linatoa fursa kwa wananchi hasa vijana kuzifahamu fikra na falsafa za mzee Karume.

Amesema kazi kubwa iliyofanywa na  hayati Karume ni pamoja na kuikomboa Zanzibar na kuiweka huru sambamba na kukubali kufanyika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao umewaunganisha Watanzania kuwa wamoja hadi leo.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mhe Steven Massato Wasira amesema hatuwezi kuzungumzia Zanzibar pasipo lumtaja Mzee Karume ambae ndie alieipigania Zanzibar na kuiweka huru kutoka katika makucha ya wakoloni.

Amesema kuwa tuna kila sababu ya kuendelea kumkumbuka Hayati Mzee Karume kwa yale mema aliyowatendea Watanzania ikiwa ni pamoja na kupigania haki na usawa, kuondosha dhuluma, ubaguzi na matabaka ya makabila na udini na kuwafanya watu wote ni wamoja na wenye haki sawa.

Mkuu wa Chuo cha Mwalim Nyerere Profesa Shadrak Mwakalila amesema Dira ya Chuo hicho ni kuwa kitovu cha utoaji wa elimu bora yenye uvumbuzi na kuendeleza thamani ya Umoja wa Kitaifa.

Amesema kuwa Chuo cha Mwalim Nyerere kampasi ya Karume Zanzibar itaendelea kuenzi mchango wa Hayat Mzee karume kupitia njia mbali mbali ikiwemo ya makongamano kwa kujikumbusha misingi aliyoijenga hasa katika kuimarisha uchumi wa nchi.

Katika Kongmano hilo Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikabidhi zawadi kwa washidi mbali mbali wa Insha iliyoakisi maisha ya Hayati karume kutoka skuli za Msingi na Sekondari za Zanzibar.

 

alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu