AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  itaendelea kutoa mashirikiano kwa Mashirika na Taasisi za kifedha zilizopo nchini ikiwemo Bank ya  NMB  ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla

alternative

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika FTARI iliyoandaliwa na Bank ya NMB hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.

Amesema kuwa Mashirika ya kifedha yamekuwa na mchango mkubwa kwa Serikali zote mbili katika  kukuza uchumi wa Taifa  kwa kutoa misaada mbali mbali  kwa Serikali na wananchi kulingana na mahitaji yao.

Mhe. Hemed amesema kuwa Bank ya NMB imekuwa mstari wa mbele katika kuyaunganisha Mashirika mbali mbali hivyo ameutaka uongozi kuendelea kutanua wigo kwa kuongeza matawai mijini na vijijini ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma zilizo bora na kwa wakati.

Aidha Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali na wananchi wameridhishwa na utendaji kazi wa Benk ya NMB  kwa kuendana na kasi ya dunia katika kutoa huduma masaa 24 kwa wananchi sambamba na kutoa gawiwo kwa seriali kuu kwa kila mwaka.

Sambamba na hayo Makamu wa pili wa Rais  ameutaka uongozi wa NMB  Benk kuwa karibu na wananchi na wateja wake katika kutoa huduma zilizo bora ili kuongeza wateja na kukuza biashara nchini.

Hata hivyo Mhe. Hemed ameupongeza uongozi wa Bank ya NMB kwa kuendeleza utamaduni wa kuwafutarisha wateje wao pamoja na watoto mayatima huku wakitaraji kupata fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu hasa kwa kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Nae Mtendaji mkuu wa Bank ya NMB Tanzania Bi. RUTH ZAIKUNA amesema Bank ya NMB imekuwa nautamaduni wa kuungana na wateja wake na wananchi kwa ujumla katika mambo mbali mbali ya kijamii ikiwemo Kuwafutarisha kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Bi Ruth amesema kuwa lengo la Ftari hio ni kukaa na wateja wao karibu katika kudumisha umoja, mshikamano na upendo baina ya Uongozi, wafanya kazi wa wateja wao ili kukuza biashara na kupiga hatua kimaendeleo.

Amesema kuwa kwa mwaka huu Bank ya NMB imeamua kuwaalika watoto yatima kwenye ftari hio  kwa lengo la kuwafanya watoto hao kujiona na wao ni sawa na watoti wengine na Taifa halijawatenga kwa kuondokewa na wazazi wao

alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu