AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.

alternative

Uongozi wa CCM Kata ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kushirikiana na uongozi wa CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar, wamempongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati, hasa mradi wa Treni ya SGR (Standard Gauge Railway), ambao umeleta suluhu kubwa kwa changamoto za usafiri wa nchi kavu nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na viongozi na wanachama wa CCM kutoka Kata ya Mwananyamala na CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar walioshiriki katika ziara ya kutembelea mradi huo.

 Ziara hiyo ilianza kwa kupanda treni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, ambapo viongozi hao walielezea kutambua na kuthamini juhudi hizo za Serikali, wakikiri kuwa mradi wa SGR umeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri nchini.

Akizungumza katika ziara hiyo, Katibu wa Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar, Bi. Msekwa Mohamed Ali, alisema kuwa kupitia ziara hiyo wamejionea kazi kubwa na nzuri iliyofanywa katika mradi wa kimkakati wa SGR, akisisitiza kuwa mradi huo umeonyesha matumizi sahihi ya fedha za walipa kodi.

 Aliwataka wananchi kumpongeza Rais Samia kwa juhudi hizo na kuendelea kumunga mkono kwa kusafiri na treni hiyo katika safari mbalimbali, ili wawe mashuhuda wa mafanikio hayo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mwananyamala, Pili Muongela, alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake kwa kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, hasa mradi wa SGR, ambao umekuwa mwarobaini wa kumaliza tatizo la usafiri nchini.

Akitoa ufafanuzi wa ziara hiyo, Katibu wa CCM Kata ya Mwananyamala, Stanly Rufini Mvungi, alisema kuwa ziara hiyo pia ilihusisha kutembelea miradi mingine, ikiwemo sekta ya utalii kupitia Mradi wa Royal Tour, ambapo walifanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Mikumi, mkoani Morogoro, na kujionea wanyama pori na vivutio mbalimbali.

 Alisisitiza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuthamini mafanikio ya miradi mikubwa ya kimkakati, kama vile Mradi wa Bwawa la Mwl. Nyerere, ambao umeleta manufaa makubwa kwa wananchi.

Ziara hiyo iliwashirikisha viongozi mbalimbali wa chama na jumuiya zake  kutoka Tanzania Bara na visiwani, na ililenga kuonyesha mafanikio ya Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya taifa.

Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.

alternative
Habari Nyingine
Albamu