Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa ni siku nne baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaapisha Mawaziri hao tarehe 9, Disemba 2024, Tunguu Zanzibar.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Waziri Bashungwa amemshukuru mtangulizi wake kwa makabidhiano ambayo yatakuwa mwongozo wa kusimamia na kutekeleza majukumu yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi.
Sambamba na hilo, Waziri Bashungwa ameshukuru Rais. Dkt Samia ambapo amesema kuwa "Niendelee kumshukuru Rais wetu na nimuahakikishie kama ambavyo alituelekeza wakati anatuapisha kwamba niendeleze pale ulipoishia Waziri Masauni”.
Aidha, Bashungwa amesisitiza suala la Watumishi wa Wizara na vyombo vyake vya usalama kufanya kazi kwa kushirikiana ili kwa pamoja kusimamia na kutekekeleza majukumu yao kikamilifu.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamadi Masauni amemueleza kuwa Waziri Bashungwa anaipokea Wizara ikiwa katika hali nzuri na hali hiyo inatokana na namna Mheshimiwa Rais Samia alivyoiwezesha kibajeti Wizara hiyo.
"Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana miongoni mwa kazi aliyoifanya ni kuiwezesha Wizara kuwa na uwezo wa kutekeleza zaidi majukumu yake." Alisema Waziri Masauni
Waziri Masauni ameeleza kuwa Wizara inaendelea na utekelezaji wa maelezeko ya Tume ya Haki Jinai ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Wananchi wanahudumiwa kwa haki, bila uonevu wala dhuluma.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
18-11-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
18-11-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
18-11-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
18-11-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
18-11-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
18-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
18-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
18-11-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
18-11-2025
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema chama hicho kitaendelea kuthamini na kuendeleza kwa vitendo mahusiano mema ya kisiasa,kijamii na kiplomasia baina yake na chama cha kikomunisti cha China (CPC).
18-11-2025