Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
Wito huo aliuatoa wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo mabalozi wa CCM Wilaya ya Amani, yaliyofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini, Amani, Zanzibar.
Dkt. Dimwa alisisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinafanya siasa za kisayansi zinazozingatia takwimu halisi za wanachama wake, ili kupata tathmini sahihi inayotoa muelekeo chanya katika kuhakikisha ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Alisema kuwa mabalozi hao wana jukumu kubwa la kufahamu kiwango cha mtaji wa chama katika maeneo yao na kuhamasisha wafuasi wa vyama vingine kujiunga na CCM.
Katika maelezo yake, Dkt. Dimwa pia alikumbusha kuwa CCM ilifanya majaribio ya mitambo yake kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, ambapo ilipata ushindi mkubwa wa zaidi ya asilimia 99.
Aliongeza kuwa hakuna chochote kinachoweza kuzuia CCM kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
“Mnapewa mafunzo haya kwa ajili ya kuwakumbusha majukumu yenu sambamba na kuwaandaa kisaikolojia kuelewa kuwa wakati wa kupambana katika vita ya kisiasa umefika.
Ni lazima mfanye kazi kwa kujiamini, uzalendo, ukweli, na kufuata maelekezo kutoka kwa viongozi wenu,” alisema Dkt. Dimwa.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kutekeleza kwa ufanisi ibara ya 5 ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 (toleo la 2022), inayoelekeza kuwa ushindi wa CCM ni lazima kwa kila uchaguzi uwe wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu wa dola.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Amani, Getrude Bonifasi, alieleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiutendaji mabalozi hao, ambao ni nguzo muhimu katika upatikanaji wa ushindi wa chama katika kila uchaguzi.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
06-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
06-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
06-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
06-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
06-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
06-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
06-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
06-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
06-12-2025
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema chama hicho kitaendelea kuthamini na kuendeleza kwa vitendo mahusiano mema ya kisiasa,kijamii na kiplomasia baina yake na chama cha kikomunisti cha China (CPC).
06-12-2025