AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi unaoendelea wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi jambo ambalo linarejesha nyuma dhmira ya Dkt. Hussein Mwinyi ya kuhakikisha anaondoa changamoto zote kwa wananchi ikiwemo ya Elimu kwa wanafuzi wa Mikoa yote ya Zanzibar

alternative

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa skuli ya Sekondari ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuitembelea skuli hio kila ifikipo mwisho wa mwezi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali imeshailipa Kampuni ya Fuchs Contraction Limited shiling Bilioni 4.08 ili kuharakisha umalizikaji wa Ujenzi wa Skuli hiyo lakini kasi ya ujenzi bado inasuasua na kupelekea wanafunzi kuendelea kufuata huduma ya elimu maeneo ya mbali na makaazi yao.

Amesema kuwa endapo Mkandarasi kutoka kampuni ya Fuchs atashindwa kumaliza ujenzi wa skuli hio na nyenginezo amabazo zinajengwa na kampuni hio kwa wakati ambao wamekubaliana katika mkataba wao itakuwa wamejinyima fursa ya kufanya kazi  ndani ya Zanzibar hasa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nane(8) na serikali haitalifumbia macho jambo hili.

Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Nane(8) inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Ali Mwinyi ni kuondoa changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na kuwekeza zaidi katika Sekta ya elimu ambayo ndio  muhimili mkuu wa maendeleo nchini.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefika katika skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la dahalia ya wanawake liloungua moto na kusababisha hasara kubwa kwa wanfunzi wanaosoma skulini hapo, na kuwataka walimu na wanafunzi kuendelea kulitunza na kudumisha usafi ndani na nje ya jengo hilo ili liweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Mhe. Hemed ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Elimu kuhakikisha ndani ya muda mfupi ujao wanaijengea uzio skuli hio ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanafunzi wanaishi hapo sambamba na kumtaka Mkandarasi kutoka Kampuni ya Faster kuhakikisha anamalizia matengenezo madogo madogo yaliyobakia ndani ya siku tano(5) ili wanafunzi waweze kuhamia na kuendelea na masomo yao katika hali ya utulivu.

Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulghulam Hussein amesema wizara imejipanga kuhakikisha inaipatia kila skuli  vifaa vya kusomea vya kisasa ili kuboresha mfumo wa elimu Visiwani ZanzibarambapoWizara imefanya ununuzi wa vifaa mbali mbali ikiwemo vitanda zaidi ya elfu moja(1000) kwa ajili ya skuli ambazo zinamadahalia  Kompyuta, Projecta, viti na meza ambavyo vyote vitagawiwa kwa skuli zote za Unguja na Pemba.

Mhe. Gulam ameiomba Serikali kuichukulia hatua ya kuipiga penalt  Kampuni ya Fuchs kwa kusababisha kuchelewa kumalizika kwa Ujenzi wa Skuli nane (8) zinazojengwa na kampuni hio jambo ambalo litatoa fundisho kwa kampuni nyengine zitakazopatiwa fursa ya kufanya kazi na Serikali ya Awamu ya Nane (8).

Kwa upande wake Mkandarasi kutoka kampuni ya Fuchs Contraction Ltd Devid Mwasomola amesema changamoto kubwa iliosababisha kishindwa kuendelea na Ujenzi wa Skuli hio ni kukosekana kwa nondo na malipo kwa ajii ya wafanyakazi hivyo ameaahidi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi hio ndani ya muda uliopangwa kwa sasa.

Katika ziara hio Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametembelea ujezi wa skuli ya ghorofa (G+3) ya  Sekondari ya Makunduchi inayojengwa na Kampuni Fuchs Contraction Limited, na kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la dahalia ya wanawake katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame liloungua moto na kusababisha athari kubwa kwa wanafunzi wanaoishi hapo mwishoni mwa mwaka jana.

 

alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu