Watanzania na waumini wa Dini ya Kiislamu kuhimizana kila wakati juu ya kuitunza amani iliopo nchini kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.
Ameyasema hayo alipokuwa akisalimiana na waumini wa Dini ya kiislamu katika Masjid KAHFI uliopo MKELE KWA BIMTORO Wilaya ya Mjini mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Alhajj Hemed amesema ili Taifa lipige hatua kimaendeleo ni lazima kuwepo na Amani na Utulivu ndani ya nchi, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi wa Tanzania na muumini wa Dini ya kiislamu na dini nyengine kuhakikisha anaienzi na kuilinda Amani iliyopo nchini kwa faida ya vizazi vya sasa na baade pamoja na Taifa kwa ujumla.
Makamu wa pili amesema zipo nchi duniani hawawezi kujumuika pamoja katika kufanya ibada kutokana na kutokuwepo kwa amani na utulivu ndani ya nchi zao hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha anaitunza tunu ya amani iliyopo kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Amesema ni lazima kujifunza kutoka kwa nchi za jiarani jinsi wanavyokosa amani kwa sasa jambo ambalo linapelekea kukosekana kwa maendeleo na kuwataka wananchi kutokubali kushawishiwa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi yetu hasa kipindi cha siasa.
Aidha Alhajj Hemed amewataka baadhi ya viongozi kuacha kutoa maneno ya uwongo na yauchochezi ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani iliyopo nchini na kuwataka kuihubiri amani wakati wote ili kupata maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed ameendelea kuwakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum wakiwemo mayatima, wajane na wazee wasiojiweza ili kuzidisha upendo baina yao.
Amesema ipo haja ya kuitumia misikiti kwa kuyatambua makundi haya muhimu ili kuweza kuyasaidia ikiwa ni njia moja wapo ya kudumisha upendo na ushirikiano na kuweka usawa wa kila mwannchi.
Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim MUHITA ALI HASSAN amewataka waumini wa dini ya Kiislam kujitathmini na kujiangalia upya katika kufanya ibada hasa katika kipindi hichi cha kuukaribisha mwaka mpya wa kiislamu siku chache zijazo.
Amesema kuwa uislamu umewataka waumini kuhimizana katika kufanya ibada pamoja na kuwa wamoja kwa kila kitu hasa katika kuipigania dini ya kiislamu ili kuweza kufikia malengo ya kuletwa hapa duniani
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
19-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
19-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
19-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
19-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
19-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
19-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
19-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
19-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
19-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
19-12-2025