SERIKLI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema itaendelea kutenga bajeti ya
mikopo kuwasaidia vijana wanaokosa fursa ya kujiunga na elimu ya juu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa, viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, Serikali imejipanga kufanikisha lengo lake hilo licha ya ongezeko la kila mwaka la vijana wanaopata sifa za kujiunga na elimu ya juu.
Alisema, Serikali imechukua jitihada mbali mbali kuimarisha ustawi wa vijana kwa kuwashirikisha kwenye sekta zote za Maendeleo ikiwemo Afya, Elimu, Kilimo, Uvuvi, TEHAMA, Ujasiriamali na michezo kwa kuwawesha kujiajiri na kuajiriwa.
Aidha, Dk. Mwinyi alieleza Serikali za SMZ na SMT zimeweka utaratibu maalum wa ajira, chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma nambari 2/2008 ambayo imetoa asilimia 21% ya Ajira kwa Vijana wa Zanzibar kwenye Sekta za Muungano.
Alisema, kwa mujibu wa taarifa ya muelekeo wa Kiuchumi ya mwaka 2022 kupitia miradi ya fedha za ahueni za UVIKO 19, jumla ya vijana 13,870 walifanikiwa kupata ajira za muda kupitia miradi iliyowekezwa na Serikali kupitia sekta mbalimbali za maendeleo.
Alieleza, mbali na jitihada za kuanzisha Wizara na Idara Maalum ya kushughulikia Maendeleo ya Vijana ili kuimarisha usimamizi na uratibu wa shughuli za Maendeleo yao nchini pia Serikali imeanzisha Sera ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2005 iliyoweka miongozo ya shughuli zote za Maendeleo na Ustawi wao.
Akiizungumzia maendeleo ya sekta ya Afya kwa vijana, Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya imekua ikishirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu ulimwengu (UNFPA) kwa pamoja wameanzisha na kuviendeleza vituo 13 vya huduma rafiki za Afya kwa Vijana kwa wilaya zote za Unguja na Pemba.
Pia, alieleza juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyoanza mradi wa ujenzi wa Vituo vya mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Vijana kwa Unguja na Pemba ambavyo vitachochea maendeleo yao kwa kuitumia taaluma watakayoipata, ikiwemo kwenda sambamba na Ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia.
Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliahidi kuanzishwa Sera mpya ya Maendeleo ya Vijana itakayozingatia mahitaji ya wakati wa sasa na ujao, alitoa wito kwa taasisi zote za Umma na binafsi, Washirika wa Maendeleo, Mabaraza ya Vijana, na Asasi za Maendeleo ya Vijana, kushiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa Sera hiyo kwa vitendo ili kufikia lengo lililokusudiwa na Serikali.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita aliiahidi Serikali kuendeleza fursa kwa vijana, kuwasimamia, kuratibu na kupunguza changamoto zinazowakabili.
Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM) Muhamed Kawaida, alipongeza juhudi za Serikali ya Dk.
Mwinyi kwa mara ya kwanza amefanikiwa kuwaweka pamoja vijana wa vyama vya mbalimbali bila kujali tofauti za itikadi zao na kueleza kuwa hatua hiyo imeendelea kuimarisha amani ya Zanzibar iliyopo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, Yunus Juma Ali aliwaasa vijana kuendeleza heshima kwenye jamii, kuvumiliana na kuyasema mambo yenye uhakika kwa kufanyia utafiti na kujiridhisha kabla ya kuzungumza.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
16-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
16-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
16-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
16-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
16-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
16-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
16-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
16-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
16-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
16-12-2025