DK. MWINYI AMEPOKEA RIPOTI YA CAG
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itawachukulia hatua za kisheria watumishi kutoka taasisi na mashirika ya Umma walioshindwa kutoa majibu kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti ya mwaka wa Fedha 2022- 2023 iliyowasilishwa na kusomwa Ikulu, Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza kwenye viwanja vya Ikulu, Zanzibar baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Kuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar, (CAG).
“Nitatataka kupata majibu kwa wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG ambao hawakutoa majibu, watoe ambao watashindwa kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa” Alilisitiza Rais Dk. Mwinyi
Dk. Mwinyi alisema, ripoti imeonesha mafanikio, changamoto na mapungufu ambayo Ofisi ya CAG iliyabainisha wakati wa uwasilishwaji wake na kueleza kwamba Serikali itachukua hatua mbali mbali zikiwemo za kiutawala na kijinai kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizowekwa.
“Kwa wale wote watakaothibitika kufanya ubadhirifu, wizi au uzembe ulioisababishia Serikali kupata hasara, utaratibu wa kuchukua hatua uko wazi” Alibainisha Dk. Mwinyi.
Alisema, kuna baadhi ya maeneo yanahitaji kuchukuliwa hatua za kiutawala na baadhi ya kuchukuliwa hatua za sheria za makosa ya jinai.
Alidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba ataikabidhi ripori hiyo kwa Mamlaka zinazohusika kwa hatua zaidi, ikiwemo Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi, Zanzibar (ZAECA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili nao waipitie kwa kina mapungufu yote hasa yaliyoashiria wizi kwaajili ya hatua zaidi kwa mujibu wa sheria.
Dk. Mwinyi alisema, ripoti za CAG ni kipimo tosha cha utendaji kwa wale wote waliopewa majukumu na Serikali kwa kufanikiwa ama kushindwa kuyasimamia katika kuitumikia Serikali.
“Utaratibu huu tuliouazisha wakuwasilisha ripoti za CAG hadharani utakuwa wadudumu, nafahamu kuwa haukuzoeleka na unawapa mashaka baadhi ya watu, nataka niwahakikishie kwa wale wenye mashaka, hili litakua zoezi la kila mwaka, na ni moja wapo ya kigezo cha uwazi na utawala bora katika uendeshaji wa Serikali yetu” Alitanabahisha Rais Dk. Mwinyi.
Hata hivyo, aliwataka watendaji na watumishi wa taasisi na mashirika ya Serikali kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Zanzibar panapokua na wajibu wa kufanya hiyo. Alisema kutofanya hivyo ni kosa kisheria na Serikali haitosita kutimiza wajibu wake.
Akizungumzia mapungufu yaliyojitokeza kwenye ripoti hiyo, Rais Dk. Mwinyi alieleza baadhi ya mapungufu hayo ni ya kiutaratibu, mengi yalisababishwa na wizi na mengine uzembe kwa baadhi ya watu.
Hivyo alieleza, kazi ya CAG kutoa taarifa na mapendekezo kwa Serikali na jukumu la kufanyiakazi ripoti hiyo ni la Serikali.
Mapema, akiwasilisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dk. Othman Abass Ali, aliishauri Serikali kuunganisha pamoja mifumo yote ya fedha ya Serikali, kwa miamala ya fedha zikiwemo fedha zilizoko Benk kuu ya Tanzania (BOT) kupitia mifumo ya Wizara ya Fedha kwa lengo la kuiwezesha mifumo hiyo, kufanya usuluhishi wa upatikanaji wa taarifa za ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa wakati sahihi.
Sambamba na kuziunganisha pamoja sekta zote za Serikali zinazofanyakazi zinazofanana katika mfumo mmoja zikiwemo, Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Kampuni ya Usafirishaji bandarini na nyenginezo ili kupata idadi kamili ya wageni na abiria wanaoondoka Zanzibar kwa lengo la kuwepo kigezo sahihi cha ukokotoaji wa ukusanywaji wa mapato yanayotakiwa kupatikana kutoka kwenye vyanzo hivyo.
Pia aliishauri Serikali kuongeza udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitenganishi, ikiwemo kufanya uteketezaji pamoja na kuvipitia vituo vyote vya afya kwa hospital zote za Wilaya, Mikoa hadi Rufaa kwa dawa zilizomo hospitalini pia kufanya vipimo vya kimaabara ili kugundua dawa na vifaa visivyo salama kwa matumizi wa binaadamu kwa kuzichukulia hatua za haraka na kuziondosha kwa kuziteketeza kwa wakati.
Akizungumzia suala la kulipa fidia kwa wananchi wanaotoa maeneo yao kwaajili ya kupisha miradi ya Serikali ya Maendeleo, CAG akiishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwalipa kwa wakati ili kuepusha malalamiko, kucheleweshewa kulipwa kwa wakati kunapunguza thamani ya fidia kutokana na kupungua kwa thamani ya fedha.
Jumla ya ripoti saba ikiwemo ya Serikali Kuu (Mawizara na taasisi zote), Mashirika na Taasisi zinazojitegemea, ripoti ya Idara Maalum na taasisi zake, ripoti ya mifumo yote ya Tehema ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ripoti ya Mashirika ya Umma, na ripoti ya Ufanisi ya miradi ya Maendeleo iliyofadhiliwa na fedha za Uviko 19 ziliwasilishwa.
Kifungu cha 112 (5) kinamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, awasilishe taarifa yote aliyoikagua na aikabidhi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa hatua nyengine. Mei 11 mwaka huu alivyanya hivyo na baadae Rais Dk. Mwinyi alimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman ambae nae aliikadhiri Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa takwa la kikatiba kwaajili ya kujadiliwa.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
22-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
22-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
22-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
22-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
22-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
22-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
22-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
22-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
22-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
22-12-2025