AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


MWINYI KUJENGA KIWANJA CHA KISASA TUMBATU

alternative

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekubali ombi lilotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma kupitia TASAF  juu ya mpango wa kujenga kiwanja cha kisasa cha michezo katika kisiwa cha Tumbatu.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Tumbatu Jongowe ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Mwinyi aliwapongeza kwa kuja na wazo hilo na kuahidi kwamba wakishafika hatua nzuri basi ataweka nyasi bandia ili kuona vijana wanacheza katika mazingira mazuri.

Mapema, Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Shughuli za Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma, alisema kuwa kwa kushirikiana na TASAF wana mpango wa kujenga kiwanja Maalum cha mpira katika Kisiwa cha Tumbatu kama ni sadaka yao katika kisiwa hicho ili kuwawekea mazingira mazuri ya michezo vijana wa kisiwa hicho.

Alisema kuwa atakaa na viongozi wa Jimbo hilo kwa kushirikiana nao katika kuona  vijana wa kisiwa hicho wanapata kiwanja kwa ajili ya michezo ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu.

Hivyo, alimuomba Rais Mwinyi kushirikiana katika ujenzi huo kwa kuwatilia nyasi bandia kama alivyoahidi katika maeneo mengine ikiwemo viwanja vya Mjini.

Habari Nyingine
Albamu