AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI TANZANIA IKULU ZANZIBAR.

alternative

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya uwekezaji ni muhimu katika ustawi wa uchumi wa Zanzibar.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo, Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess aliefika kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi hapa Tanzania. Alisema, Zanzibar bado ina fursa pana ya kuendelea kunufaika na uwekezaji kutoka Ujerumani kutokana na ushirikiano mwema ulipo baina yao.“Bado tuna fursa kubwa ya kuendelea kushirikiana na Ujerumani katika kukuza uwekezaji na kuongeza watalii wengi, Zanzibar. Tunashajihisha sana suala la uwekezaji sababu ndio kiungo kikubwa kwa uchumi wa Zanzibar” Alifafanua Dk. Mwinyi.Rais Dk. Mwinyi alieleza, Ujerumani imetoa mchango mkubwa kwa kuiinga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia sekta ya maji safi na salama ambayo aliieleza kuwa ni sekta muhimu kwa ustawi wa watu wa Zanzibar.

Pia Dk. Mwinyi aliishikuru Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano wanaendelea kuutoa kwa SMZ kupitia Sekta ya Afya na Michezo pamoja na kushajihisha watalii wengi raia wa Ujerumani wanaoingia Tanzania.Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Hess alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa weledi wake wa kuridhia uongozi wake wa Serikali ya Umoja wa kitaifa pamoja na hatua alizozichukua za kuunda kamati ya maridhiano kitaifa kati ya Chama tawala CCM na cha upinzani ACT Wazalendo, akimsifu kwa jitihada zake za kuendelea kudumisha amani na utulivu wa kisiasa, Zanzibar.

Wakati huo huo, Balozi Hess alimtambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Balozi wa heshima Dk. Jenny Bouraima atakaeiwakilisha Ujerumani na kufanya kazi zake hapa Zanzibar.Akizungumza mara bara baada ya utambulisho huo, Dk. Jenny ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zaznzibar na kuahidi kushirikiana nayo bega kwa bega hasa kwenye suala zima la kuitangaza zaidi Zanzibar kupitia sekta ya utalii pamoja na kuiunga mkono sera ya Uchumi wa Buluu kwa kuwashajihisha zaidi Wajerumani kuja Zanzibar kuwekeza kupitia rasilimali bahari.

alternative
Habari Nyingine
Albamu