AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS DK.MWINYI ASAINI SHERIA MPYA ZINAZOGUSA WANANCHI NA HAKI ZAO

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kusainiwa kwa sheria mpya itaondoa changamoto ambazo zilikuwa vikwazo katika kufikia malengo ya kimaendeleo. 

Amesema sheria hizo mpya ni Sheria mpya ya Mahkama ya Kadhi Zanzibar, Sheria mpya ya Ukaguzi wa Umma, Sheria mpya ya Uwekezaji Zanzibar, ambayo ni sheria bora kwa mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji nchini, Sheria ya kuweka masharti ya  utoaji leseni udhibiti na usimamizi wa huduma ndogo za fedha kwa ajili ya kudumisha utulivu, usalama na ubora wa huduma hizo.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati wa  hafla ya utiaji saini wa sheria mpya nne viwanja vya Ikulu Zanzibar tarehe: 01 Februari 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Sheria zilizosainiwa zimepita katika hatua mbalimbali ikiwemo kufanyika kwa utafiti wa kina na ukusanyaji wa maoni ya wadau Unguja na Pemba kabla ya kuwasiilishwa  Baraza la Wawakilishi na kujadiliwa kwa mfumo wa demokrasia shirikishi.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa ni jambo la kihistoria kusainiwa kwa sheria mpya nne hadharani kwa wakati mmoja.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Sheria zote nne zilizosainiwa zinagusa moja kwa moja maslahi ya wananchi na haki zao ikiwemo kuimarisha miongozo ya mifumo jumuishi ya  kusimamia shughuli zote za uwekezaji, kupanua wigo wa kazi za ukaguzi  ili kufikia ngazi za kitaifa na kimataifa, kubaini na kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma, kukabiliana na vitendo vya rushwa, kuzuia matumizi  mabaya ya mifumo inayoathiri utekelezaji wa kazi za ukaguzi. 

Rais Dk.Mwinyi amezitaka taasisi za sheria kufanya mapitio sheria zinazokwaza kasi ya maendeleo katika maeneo ya mafuta na gesi asilia.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu