Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema uwepo wa Maonesho ya Wiki ya elimu ya juu nchini yamekuwa yakiziweka pamoja Taasisi, vyuo na wadau wa elimu ya juu kwa lengo la kutangaza fursa mbali mbali kwa wanafunzi wanaosoma na wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu vya ndani na nje ya Nchi
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Tano(5) ya wiki ya elimu ya juu Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mhe. Hemed amesema kupitia maonesho ya wiki ya elimu ya juu wanafunzi hupatiwa fursa mbali mbali za kimasomo ikiwemo upatikanaji wa mikopo, namna ya kujiunga na vyuo vya ndani na nje ya nchi na kutoa hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na kujiendeleza katika ngazi ya elimu ya juu.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Sera na Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imekuwa ikichukua hatua mbali mbali za uboreshaji wa elimu ikiwemo kuweka mageuzi makubwa kuanzia ngazi ya maandalizi hadi elimu ya juu kwa kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa baada ya kumaliza masomo yao.
Aidha Serikali imeongeza Bajeti ya Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu Zanzibar kutoka fedha za Kitanzania shilingi Bilioni 26.95 kwa mwaka wa fedha 2024 hadi kufikia Bilioni 30.5 kwa mwaka 2025 ambazo zitakwenda kuwanufaisha wanafunzi zaidi ya 7,367 ambapo kwa mara ya kwanza wanafuzi 1,000 wa ngazi ya Diploma watanufaika pia na mikopo hio.
Amefahamisha kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ikiwemo kuwapatia Bima ya Afya pamoja na kuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wote wanaosoma Vyuo vya Zanzibar na vyuo vya Tanzania Bara.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoa wito kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kuitumia vyema wiki ya maonesho kwa kujielimisha juu ya upatikanaji wa fursa mbali mbali za elimu ndani na nje ya nchi na kuwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidiii na kuzitumia vyema fursa wanazozipata pamoja na kuepuka kutumika kwa misingi yoyote ambayo itapelekea kuvuruga umoja na amani iliyopo nchini
Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Mwinyi inafanya kazi kubwa na nzuri katika kuimarisha miundombinu ya elimu inayopelekea kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu jambo ambalo linaendelea kuiletea heshima zanzibar.
Mhe. Lela amesema ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha sita unaongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia asilimia 99.5% kwa mwaka 2024, ambapo zaidi ya wanafuzi 3,387 wamepata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu na wote wanatarajiwa kujiunga na vyuo vikuu mbali mbali ndani na nje ya nchi, hivyo kupitia maonesho ya juma la elimu ya juu yatawasaidia katika kufanya udahili wa vyuo na kupata taaluma juu ya kupata mikopo ya elimu juu iatakayowawezesha kusoma pasipo na changamoto ya aina yoyote.
Akisoma taarifa ya kitaaluma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Naibu katibu Mkuu Utawala (WEMA) Khalid Massoud Waziri amesema lengo kuu la maonesho hayo ni kuimarisha mashirikiano baina ya Taasisi za Elimu, Vyuo na Mabenki ili kuhakikisha Sekta ya Elimu nchini inaendelea kuimarika na kiwango cha ufaulu kuzidi kuongezeka siku hadi siku.
Khalid amesema maonesho hayo ya juma la Elimu ya juu yanazidi kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka huu washiriki wameongezeka kutoka washiriki 17 mwaka 2020 hadi washiriki 77 mwaka 2024 na kutoa fursa kwa wanafunzi kupata kujua ni namna gani wanaweza kujiunga na vyou vikuu vya ndani na nje ya nchi samabamba na kupata kujua ni namna gani mwanafuzni anapata fursa ya kufanya maombi ya mikopo kwa taasisi husika.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametembelea Mbanda ya washiriki wa maonesho ya juma la Elimu ya juu na kupata elimu na huduma zinazotolewa katika mabanda hayo
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
29-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
29-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
29-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
29-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
29-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
29-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
29-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
29-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
29-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
29-12-2025