Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ametoa agizo kwa uongozi wa Kampuni ya Lancet kuhakisha ndani ya mwezi mmoja kitengo cha wagonjwa walio katika uangalizi maalum (ICU) katika hospitali ya Wilaya ya Magharibi “B” Mwanakwerekwe Ijitimai kinatoa huduma ili kuondoa usumbufu wa ongezeko la wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya utowaji na upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi katika hospital ya Wilaya ya Magharibi “B” Mwanakwerekwe Ijitimai na Hospital ya Taifa ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema kuwa Kampuni ya Lancet ina wajibu wa kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatika kwa ubora na haraka kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali zote za Wilaya ili kuondosha msongamano wa wagonjwa katika hospital za Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Awamu ya Nane imelipa kipaombele suala la kuboresha miundombinu ya Afya ili kuzidi kutoa huduma bora za kitabibu kwa Wananchi hivyo wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi katika kuwaletea maendeleo ikiwemo upatikanaji wa huduma bora za Afya.
Mhe. Hemed amewasisitiza madaktari kudumisha nidhamu katika kazi kwa kufuata miiko, miongozo na maadili ya kazi zao na kuachana na tabia ya kuwatolea lugha chafu wagonjwa hasa wahuduma za Dharura ili kuendelea kuilinda heshima ya wananchi ambapo Serikali haitamvumilia mtu yoyote atakae kwenda kinyume na maadili ya kazi na itamchukulia hatua za kisheria na kinidhamu kwa haraka .
Aidha Makamu wa Pili wa Rais amezitaka kampuni ya Lancet na NSK zinazotoa huduma katika hospital za Wilaya na Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kuhakikisha changamoto zote za vifaa, wataalamu na kiutendaji zinapatiwa ufumbuzi kwa haraka ili kupunguza malalamiko kwa wananchi ambao wameipa Imani Serikali yao ya kiwatumikia na kuwaletea maendeleo.
Sambamba na hayo amewasisitiza wananchi kuendelea kuzitumia Hospitali za Wilaya katika kutafuta matibabu ambazo zinatoa huduma zote za kitabibu ili kupunguza wingi wa wagonjwa katika hospitali za Rufaa.
Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa Serikali kuu itahakikisha inatatua chamgamoto zote zinazoikabili Sekata ya Afya zitapatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuendelea kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dkt. MUHIDDIN ABDI MAHMOUD amesema katika kupunguza changamoto ya wataalamu katika Hospitali za Wilaya na Rufaa Wizara ya Afya imeamua kusomesha wafanyakazi wake kwa kuwalazimisha kusomea zile kada ambazo zina upungufu wa madaktari ili kuweza kutoa huduma zilizo bora na kwa wakati.
Amesema kuwa Wizara ya Afya imepanga kuandaa utaratibu wa kuwashauri na kuwashawishi wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu kusomea kozi ambazo zina uhaba wa wataalamu ikiwemo ICU, Ganzi na Usingizi pamoja na Huduma za dharura ili kuweza kulisaidia Taifa kupata wataalamu wazawa.
Kwa upande wao wananchi waliofika hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea hospitali za Wilaya na kuwasogezea huduma za matibabu karibu na makazi yao zinazotoa huduma bora na kwa wakati sambamba na kuwashukuru Madaktari kwa huduma bora wanazowapatia wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
15-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
15-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
15-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
15-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
15-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
15-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
15-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
15-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
15-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
15-12-2025