AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


DKT. DIMWA AZUNGUMZA NA MASKANI YA CCM MWEMBE MADEMA

alternative

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed (Dimwa) amesema, anatambua na kuthamini mchango unaotolewa na maskani za Chama cha Mapinduzi katika kukupigiania chama na kukiletea ushindi.

Dk. Dimwa aliyasema hayo jana wakati alipokutana na wanamaskani ya CCM ya Mwembe Madema waliofika katia ofisi za Naibu Katibu Mkuu huyo huko Kiswandui Mjini hapa kwa lengo la kujitambulisha.

Alisema, kicha ya maskani za Chama cha Mapinduzi kuwa na mchango mkubwa ndani ya CCM lakini zimekuwa ni chachu ya kuongeza wanachama wa Chama cha Mapinduzi.

"Najua mchango wa maskani katika Chama cha Mapinduzi, najua tabu mlizozipata wakati wa uchaguzi na wakati woe ambao mlikuwa mnakitetea Chama na serikali kwa ujumla pindi inaposemwa vibaya," alisema

Alisema, imani yake kubwa ni kuona kwamba kazi za chama zinaenda vizuri kuanzia katika maskani za CCM na kusema kuwa wakiednelea kuungana kwa pamoja basi uchaguzi wa mwaka 2025 utakuwa mwepesi sana.

"Kikubwa tu naomba mnipe mashirikiano ya kitosha nyinyi maskani ya Mwembe Madema na maskani nyengine zote za Chama cha Mapinduzi ili kukipeleka mbele Chama chetu cha Mapinduzi," alisema.

Aidha Dk. Dimwa alisistiza swala zima la amani katika nchi na kusema maridhiano yao na vyama vya upinzani waendelee nayo kwa sababu katiba ndivyo inavyosema kuwe na serikali ya umoja wa kitaifa ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.

Alisema, katika hotuba zale amekuwa akisisitiza sana kutokukubaliana na baadhi ya viongozi wa serikali ambao wana wabeza wanachama wa Chama wa cha Mapinduzi.

Alisema, ana imani sana na wana CCM wote na yeye ndiyo mtumishi wao kwa sasa hivyo atahakikisha kuwa anawatumikia vizuri.

Mbali na hayo alisema, nafasi aliyopewa na unaibu Katibu Mkuu wa CCM hakupata kwa uhodari wowote bali amepata nafasi hiyo baada ya wana CCM kumuamini.  

Hivyo alihidi kutenda uadilifu katika nafasi yake hiyo na kuitumikia kwa nguvu zake zote na kuwataka kumpa ushirikiano wao kuanzia ngazi za matawi, shina pamoja na kwenye maskani.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Maskani ya Mwembe Madema Najma Balel Abdallah alisema, lengo la kuonana na Naibu Katibu Mkuu huyo ni kujitambulisha na kumpongeza kwa kuteuliwa na Chama kushika nafasi hiyo.

Alisema, wapo tayari kumpa kila aina ya ushirikiano Naibu huyo katika kukijenga Chama cha Mapinduzi.

Habari Nyingine
Albamu