RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kuna haja kwa Zanzibar kuongeza vivutio vingi vya utalii kwa kubuni matukio maalumu ya kuwavutia wageni wengi na kuviimarisha vivutio vya asili vilivyomo Tanzania.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kuna haja kwa Zanzibar kuongeza vivutio vingi vya utalii kwa kubuni matukio maalumu ya kuwavutia wageni wengi na kuviimarisha vivutio vya asili vilivyomo Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Dk. Samia, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa Tamasha la nane la Kizimkazi, huko uwanja wa Paje Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais Dk. Mwinyi alisema tamasha hilo linatoa fursa yakuendeleza utalii na kuutangaza mkoa wa kusini kiutalii na Zanzibar kwa ujumla kwa kufungua fursa nyingi za maendeleo ikiwemo biashara, uwekezaji na uchumi.
Alieleza matarajio yake ya baadae kwa tamasha hilo kuweka hitoria nyengine ya mkoa wa Kusini Unguja kwa kuongeza fursa nyingi za Utalii, uwekezaji na maendeleo ya biashara.
Sambamba na kueleza tamasha hilo mbali na kuongeza vivutio vya utalii vya ndani ya mkoa huo kama tukio la asili la ‘mwaka kogwa’ lakini kuendelea kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kuendeleza umoja na mshikamano wa Watanzania kwa pande zote za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwakutanisha pamoja kwa amani na upendo kupitia Tamasha la Kizimkazi ambako wasanii wengi, wananchi, taasiisi mbalimbali za binafsi, wadau wa maendeleo, wajasiriamali, wenyeji na wageni kukutana na kufurahika kwa pamoja.
Pia alieleza tamasha hilo limeendelea kuezi na kuimarisha utamaduni wa Tanzania kwa kuvienzi vyakula vya asili, kuimarisha makongamano, michezo, burudani na kuwawesha vijana kiuchumi kwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kukuza biashara, aidha, Dk. Mwinyi alieleza fursa za makampuni binafsi kuwekeza miradi mikubwa zikiwemo taasisi binafsi, tasisi za fedha na benki kutanua matawi yao kusini Unguja kutokana na Tamasha la Kizimkazi.
Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliipongeza Serikali ya Mkoa wa Kusini Unguja na kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kizimkazi kwa kuelendeza juhudi za Rais Dk. Samia kwa kulienzi tamasha hilo.
Akizungumzia fursa za Uchumi wa Buluu na uwekezaji wa biashara, Rais Dk. Mwinyi alisema Mkoa wa Kusini Unguja umebarikiwa bahari na eneo kubwa la wazi kwa wilaya zake zote mbili za Kati na Kusini mwa Mkoa huo na kueleza kupitia Tamasha la Kizimkazi na fursa zinazotoka huko, sekta ya uvuvi itaimarika zaidi kwa kilimo cha kisasa cha mwani na kuongezeka tija kwa fursa nyingi za utalii kuendelea kufunguka.
Akitoa salam za mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Unguja Rashid Hadidi aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wanatoa kukuza maendelo ya mkoa huo kwa sekta zote ikiwemo kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara za kisasa, ujenzi wa hospitali kubwa za Wilaya zenye mashine na vifaa tiba vya kisasa, skuli za ghorafa pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa matangi matatu makubwa ya maji safi yenye uwezo wa kuchukua lita milioni 10 ambayo yatasaidia kusambaza maji kwa mkoa wote wa Kusini Unguja.
Tamasha la Kizimkazi liliasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan miaka nane iliyopita likiwa na lengo la kuunganisha umoja, ushirikiano na mshikamo wa Watanzania wa Mkoa wa kusini Unguja na Tanzania yote bila kujali tofauti za asili na siasa zao.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
20-11-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
20-11-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
20-11-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
20-11-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
20-11-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
20-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
20-11-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
20-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
20-11-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
20-11-2025