RAIS DK. MWINYI TUMBATU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaahidi wananchi wa kisiwa cha Tumbatu kwamba serikali itajenga hospitali yenye hadhi ya hospitali ya Wilaya katika kisiwa hicho ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa urahisi.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo katika muendekezo wa ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipofika kisiwa kidogo cha Tumbatu kwa ajili ya ufunguzi wa madarasa, kugawa boti kwa wavuvi na wakulima wa mwani pamoja na kuweka jiwe la msingi Tangi la Maji.
Alisema kutokana na ugumu wa mazingira yaliyopo katika kisiwa hicho wakati umefika kuwa na hospitali kubwa ya wilaya ndani ya Tumbatu ambayo itaondosha usumbufu wa wakaazi wa kisiwa hicho.
"Ninayo habari kwamba watu wa kisiwa hicho wanapoumwa au wajawazito wasafirishwe kwenda upande wa pili na wakati mwengine vyombo vinakuwa havipo au hali ya hewa ya bahari inakuwa ya nguvu na watu wanapoteza maisha hivyo, serikali itajenga hospitali yenye hadhi ya Wilaya inayofanya upasuaji ili huduma za afya zipatikane huku huku bila ya kuvuka maji," aliahidi.
Aidha, Rais Mwinyi aliwahidi wananchi wa kisiwa hicho kuwajengea gati ili kuondosha changamoto ya usafiri wanayokabiliana nayo hivi sasa.
Alisema imefika wakati kuhakikisha wanajenga gati nzuri ili kuona wananchi wanafanya safari zao kwa uhakika na usalama wao .
Rais Mwinyi, aliwahidi wananchi wa kijiji hicho kwamba serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara iliyopo katika kisiwa hicho kwa kiwango cha lami na kuweka mazingira mazuri.
Alisema tayari Wizara ya Ujenzi imeshaiweka kwenye bajeti na kuahidi kwamba Serikali itatafuta fedha kuhakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami.
Akizungumzia uiamarishaji wa mazingira ya elimu, Rais Dk .Mwinyi alisema Serikali itaendelea kujenga madarasa ili kupunguza idadi ya watoto madarasani.
Alisema mpango huo utajumuisha skuli ya Maandalizi Msingi na Sekondari ambapo Tumbatu itajengewa skuli ya ghorofa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuona wanasoma katika mazingira mazuri na rafiki kwa kuweka vifaa vya kujifunza na kufundishia.
Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha inapunguza idadi kubwa ya wanafunzi madarasani kutoka 90 na kushuka chini hadi wanafunzi 40.
Mbali na hayo aliahidi kuzifanyia kazi changamoto za skuli hizo na kuhakikisha serikali inachukua jitihada za kuwaweka vifaa ili kufanya kazi inavyotakiwa na kuahidi kwamba serikali itawaongezea maslahi ya walimu.
Kwa upande wa sekta ya maji, Rais Mwinyi, alisema serikali imejenga tangi la lita milioni moja ili huduma hiyo iweze kupatikana kwa ufanisi zaidi.
"Ninazo taarifa kwamba maji Tumbatu yanatokea upande wa pili lakini yanasukumwa moja kwa moja hakuna sehemu ya uhifadhi na pampu zikiharibika watu hawana maji hivyo tangi tulilojenga linakuja kuondosha changamoto hii kwa madhumuni ya kuhakikisha pale inapojitokeza hitilafu basi yapo maji yaliyohifadhiwa na maji yasikosekane kwa kipindi kirefu," alibainisha.
Rais Dk. Mwinyi katika suala zima la kuwawezesha wananchi Kiuchumi, alisema serikali ina mpango maalum ya kuwawezesha wavuvi na kuwapatia mikopo hivyo aliwaomba kuchangamkia fursa hizo ili kujiondoa na umasikini unaowakabili.
Alikipongeza Chuo cha Mafunzo na mkandarasi aliyejenga tangi la maji kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kisiwa hicho na kuwaahidi kwamba watashirikiana katika kazi nyengine alizoziahidi katika kisiwa hicho.
Aliwapongeza wananchi wa kisiwa hicho kwa kumpa kura nyingi na kuwaahidi kwamba wategemee wakandarasi hao hawatoondoka na wataendelea kutekeleza yale aliyoyaahidi kama Ilani ya Uchaguzi ya CCM inavyoelekeza.
Mapema, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohammed Mussa alimpongeza Rais Mwinyi kwa jitihada kubwa anazozichukua katika kuimarisha sekta ya elimu na kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na yenye kuvutia.
Mwakilishi wa Jimbo hilo, Haji Omar Kheir alimshukuru Rais Mwinyi kupitia Wizara ya Elimu kwa kujenga madarasa hayo ambayo yatasaidia wanafunzi wa msingi katika kuondosha changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi madarasani.
Akitoa shukurani zake kwa upande wa sekta ya maji, alisema tangi hilo la maji ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kisiwa hicho cha Tumbatu na kutegemea maendeleo makubwa yatakayoendelea kupatikana katika kisiwa chao.
Katika ziara hiyo, huko kiswani Tumbati Rais Mwinyi pia, aligawa boti za uvuvi kwa wavuvi na wakulima wa mwani 35 ambapo hadi CRDB imetoka boti 129 kwa Unguja na Pemba zilizogharimu shilingi bilioni 1.8.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
24-10-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
24-10-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
24-10-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
24-10-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
24-10-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
24-10-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
24-10-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
24-10-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
24-10-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
24-10-2025