AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


DK. MWINYI -  SASA NI WAKATI WA KUJENGA CHAMA CHETU

alternative

Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar, ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema wakati umefika CCM kutumia rasilimali za Chama zilizopo ili kuendelea kujiwezesha kiuchumi ikiwemo kutatua changamoto za uchakavu wa majengo na posho kwa watendaji.

 

 

Akizungumza na watendaji wa ngazi mbalimbali wakiwemo mabalozi, wajumbe wa halmashauri ya mkoa wa magharibi Kichama ikiwa ni mara ya kwanza tokea kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Piccadilly Kombeni

 

 

Alisema, kumekuwa na rasilimali nyingi katika chama lakini bado hazijatumika ipasavyo hali inayochagia kuwepo kwa maslahi duni ya watendaji hivyo amewataka watendaji kulisimamia suala hilo ili kuona masuala hayo yanakaa sawa.

 

 

Aidha aliwataka viongozi wa majimbo kurudi katika majimbo yao kwani kumekuwepo baadhi ya viongozi hao, kugombana wenyewe kwa wenyewe jambo ambalo linaharibu utekelezaji wa ilani ndani ya jimbo na kupelekea kuwagawa wanachama, hivyo ameitaka sekretariet ya chama kuwaita kabla ya kusubiri siku za uchaguzi kufika

 

 

Akizungumzia makundi ndani ya Chama, Dk. Mwinyi, amewataka wanachama kuachana na makundi na waendelee kufanya kazi kwa ushirikiano kwani makundi yamekuwa yakiathiri chama.

 

 

Pamoja na hayo, aliiagiza sekretariet ya chama kuandaa mafunzo kwa viongozi wa chama waliochaguliwa kupitia ngazi zote ili kutambua wajibu wao na majukumu yao ya kiutendaji.

Aliwataka viongozi hao, kuengeza wanachama wapya pamoja na kuhamasisha na ulipaji wa ada ili kuimarisha uhai wa chama kwani uhai wa chama ni kuengeza idadi ya wanachama wapya.

Akizungumzia utekelezaji wa ilani, Rais.Dk. Mwinyi, alisema ilani ya mwaka 2020-2025 kwa sasa imefikia nusu kwani katika kipindi cha miaka miwili miradi mbalimbali wameitekeleza ikiwemo huduma za kijamii, ikiwemo Afya, Elimu, barabara na huduma za maji safi na salama ambapo baadhi ya sekta zimeshavuka lengo lililoelekeza katika ilani ya uchaguzi.

Akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Naibu, Katibu wa Chama cha CCM Zanzibar, Dk. Mohamed Said Mohamed ( Dimwa), alisema, CCM hakitajibu maneno ya wanaotaka kuchafua amani ya nchi hivyo CCM itaendelea kujibu kwa hoja vitendo ikiwemo kuwapatia wananchi maendeleo yaliyofikiwa nchini chini ya uongozi wa Rais, Dk. Mwinyi.

"CCM, hatutajibu porojo zao wapinzani sisi kawaida yetu tunatekeleza ilani ya CCM na majibu yetu nyote tunajibu kupitia maendeleo yaliyofikiwa chini ya uongozi wa makamu mwenyekiti wetu" alisema.

Pamoja na hayo, aliwasihi baadhi ya viongozi kuacha kuwabeba mikoba wagombea wakati bado wa uchaguzi haujafika na kusisitiza kuachwa viongozi waliokuwepo kufanya kazi ya utekelezaji wa ilani na endapo kiongozi atakayebainika hativumiliwa katika chama.

"Wakati wa demokrasia ikifika watakuwa na haki ya kuendelea kugombea na hatozuiliwa mtu yoyote ila kwa sasa tutakula nao sahani moja"

Akitoa salam za Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkuu wa Mkoa huo, Idrissa Kitwana Mustafa, alisema Serikali ya mkoa imekuwa ikishirikiana na serikali hasa katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025 katika upatikanaji wa maendeleo kwa wannachi wote bila ya ubaguzi.

Habari Nyingine
Albamu