AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


Waumini wa dini ya Kiislamu na wazanzibari kwa ujumla wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwaombea dua viongozi wakuu wa nchi ili waweze kuleta maendeleo na kuyatekeleza kwa vitendo yale yote waliyoyaahidi kwa wananchi wao

alternative

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid SUNNI HANAFII  MKUNAZINI  mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema wazanzibari na waumini wa dini zote wana wajibu wa kuwaombea dua viongozi wakuu ili kuzidi kuwatelete maendeleo na  kuwatekeleza mambo yote muhimu ambayo wananchi wanastahiki  kupatiwa kutoka kwa viongozi wao kama vile anavyotekeleza kwa vitendo Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuwa kila mzanzibar na mtanzania anahitaji maendeleo kwenye sekta zote zikiwemo barabara,maji safi na salama,afya na mengineyo jambo ambalo ndio dira ya viongozi wakuu kuwarahisishia wananchi wake wa kupata kila wanachokihitaji kwa ubora na kwa wakati.

Alhajj Hemed amesema serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Mwinyi ipo salama na viongozi wake wanafanya kazi kwa kushirikiana wakiwa na lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia sekta zikiwemo barabara, maji safi na salama ,elimu na mengineyo bila ya ubaguzi wa aina yoyote kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Sambamba na hayo  Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar na watanzania kwa ujumla kuendelea kuitunza na kudumisha amani na utulivu uliyopo nchini kwa kutambua kuwa amani ndio msingi wa maendeleo katika nchi yoyote duniani, hivyo ni lazima kuendelea kuitunza na kuilinda amani tulinayo ili kuweza kuwavutia wawekezaji kutoka nchi mbali mbali kuja kuekeza nchini.

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh MAHSEIN WAHID amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kushikamana katika kuitetea dini ya Allah (S.W) na kuirithisha kwa vizazi vyetu jambo ambalo litawasaidia kufikia lile lengo waliloletewa duniani la kumcha Mwenyezimungu.

Amesema kuwa suala la kuhimizana kufanya ibada na kuchuma chumo la halali ni wajibu wa kila muumin wa dini ya kiislamu, na kuwataka kutambua lengo la kuumbwa wanadamu ni kumcha Allah kwa kufuata mazuri yakiyofanywa na  mtume Muhamad (S.A.W) ambayo  yataongeza mapenzi baina yao.

alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu