Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Viwanja vya ndege ni sehemu muhimu sana kwa ukuwaji wa uchumi wa Zanzibar ambayo inategemea zaidi shuhuli za utalii ambazo zinakwenda sambamba na uwepo wa miundombinu mizuri ya viwanja hivyo.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali inayojengwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibari.
Mhe. Hemed amesema kuwa viwanja vya ndege ni milango mikuu ya nchi yoyote ile duniani inayotumika kwa kusafirishia wageni ambao huchangia kwa kiwango kikubwa kukuwa kwa uchumi na kuongezeka kwa pato la nchi husika.
Amesema kuwa utakapokamilika ujenzi wa Miradi ya Viwanja vya ndege vya Terminal One na terminal two na eneo la biashara lililopo terminal three vitaondoa changamoto ya msongamano wa abiria wanaokaa muda mrefu kusubiri kuhudumiwa sambamba na kuongezeka kwa uwezo wa kutoa huduma bora na za haraka jambo ambalo litapelekea wageni wengi kuendelea kuitembelea Zanzibar mara kwa mara.
Makamu wa Pili wa Rais amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege kuhakikisha kila penye uwezekano wa kupatikana kwa kodi kuhakikisha kodi hio inakusanywa na kuingia Serikalini ili kuendelea kuimarisha na kuboresha huduma mbali mbali za kijamii kwa wananchi wa Zanzibar.
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa ushirikano kwa kampuni zote zinazojenga miradi mbali mbali nchini ikiwemo kampuni ya Estim Constraction Ltd inayojenga miradi ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar ili kuhakikisha wanakabidhi miradi hio kwa wakati uliopangwa na kwa kuzingatia viwango na ubora wa hali ya juu.
Nae Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Dkt Khalid Salum Muhammed amesema uchumi wa Zanzibar unategemea zaidi Utalii hivyo ni lazima kuimarisha miundombinu ya kimkati ikiwemo viwanja vya ndege ili kuhakikisha Utalii unakuwa kwa kasi zaidi na pato la nchi linaongezeka kupitia wagemi wanaoingia Zanzibar.
Dkt. Khalid amesema ujenzi wa miradi hio inaendelea vizuri na hakuna changamoto yoyote hadi sasa ambayo itasabisha kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa miradi hiyo sambamba na kuahidi kuwa uongozi wa wizara utahakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa kiwango kilichokusidiwa ili kufikia malengo ya Serikali iliyojiwekea.
Kwa upande wake mshauri elekezi kutoka kampuni ya Anova Consult Ltd Muhandisi IBRAHIM GASPER amesema kuwa hadi sasa miradi yote inakwenda vizuri na ipo ndani ya wakati ambapo amemuhakikishia Makamu makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa watakabidhi miradi hiyo ndani ya muda uliopangwa na kwa kuzingatia viwango vya hali juu.
Gasper ameushukuru uongozi wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Mamlaka ya Viwanja vya ndege kwa ushirikiano mkubwa wanaowapatia jambo ambalo linawapa ari ya kufanya kazi kwa haraka na kukamilisha ujenzi huo kabla ya wakati uliopangwa kwa maslahi mapana ya wananchi wa Zanzibar.
Katika ziara hio Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekagua UKARABATI WA JENGO LA TERMINAL ONE , UJENZI WA GENGO LA TERMINAL TWO pamoja NA UJENZI WA SEHEMU YA BIASHARA ILIYOPO TERMINAL THREE.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
14-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
14-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
14-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
14-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
14-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
14-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
14-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
14-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
14-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
14-12-2025