AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WASTAAFU NA WAZEE ZANZIBAR (JUWAZA)

alternative

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amezitaka mamlaka husika zinazoshughulika na masuala ya pechni na penchini jamii kwa wazee, kurekebisha na kuboresha mifumo yao ili zoezi la utoaji wa penchi kwa mwezi Julai mwaka huu kuanza bila ya kikwazo chohote.

Alizitaka mamlaka hizo kujitahidi kumaliza zoezi la usajili na uhakiki wa masuala yote muhimu yanayowahusu wazee hao yakamike ndani ya mwezi huu wa Juni ili ifikapo Julai kusiwe na kasoro zozote zitakazowakosesha wazee kupata haki yao ya pencheni.

“Nisingependa hata kidogo kwa nia njema tuliyokuwa nayo ya kuwasaidia wazee, halafu usikie Julai imefika, huyu hajapata, huyu kakosa kitambulisho, itakua hatuja wasaidia wazee” Alitahadharisha Dk. Mwinyi.

Dk. Mwinyi alitoa maagizo hayo alipozungumza na Jumuiya ya Wazee na Wastaafu, Zanzibar (JUWAZA), Ikulu – Zanzibar waliofika kumpongeza kwa hatua yake ya kuwajali na kuwaongezea pencheni na pencheni jamii.

Akizungumia changamoto ya vitambulisho kwa wazee hao hasa wakati wakupata haki zao za msingi, Rais Dk. Mwinyi alizishauri mamlaka husika kurasimisha baadhi ya vitambulisho kwa wazee hao ili wapate haki zao zote kwa wakati yakiwemo masuala ya jamii.

Alishauri kuwe na utaratibu mzuri kwa wazee hao kupata haki zao kwa wakati kusiwe na urasimu na kuwanyima haki zao za msingi.

“Hakuna ubaya wa kurasimisha vitambulisho, sio lazima vitumike “ZAN ID” au “NIDA” katika kuwapatia wazee haki zao, kama wengine hawana vitambulisho hivyo, kuwe na utaratibu kurasimisha ama kuanzishwe vitambulisho maalumu vya wazee vitakavyowaunganisha na huduma zao zote zikiwemo pensheni, pencheni jamii na masuala ya kijamii ikiwemo usafiri, afya na wepesi wa kupata huduma nyengine” alifafanua Dk. Mwinyi.

Pia Rais Dk. Mwinyi, alizishauri mamlaka zinazosimamia pencheni za wazee kushirikiana na jumuiya hiyo ya Wazee ili kubaini wazee wanaozidi ama kupungua kwenye uhakiki wao.

Alieleza kuna haja ya Taasisi za Serikali zinazoshughulikia masuala ya wazee, kukaa pamoja na kuongeza ushirikiano baina yao na JUWAZA ili kupata takwimu sashihi zinazowahusu wazee wote nchini.

Aidha, aliwaahidi wazee hao kwamba atatoa maagizo kwa uongozi wa Wizara tatu za Serikali zikiwemo Fedha, Ustawi wa Jamii na Afya, ili kwakae pamoja na wazee hao kwa lengo la kujadiliana na kuondoka na mipango mizuri Imarisha ustawi wa wazee hao kwa sasa na baadae.

“Niombe na maelekezo nitatoa, kwa Wizara tatu za Serikali, mukutane na tumu za uongozi wa Wizara ya Fedha, Ustawi wa Jamii na Afya, mjadiliane ili muondoke na mpango mzuri wa kuyafabya haya” Alisisitiza Dk. Mwinyi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu wa (JUWAZA) Salma Kombo Khamis aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapatia wazee wa Zanzibar daktari maalum atakaeshughulikia masuala ya wazee kwenye hospitali kuu ya Mnazi Mmoja (Geriatrician) pamoja na wauguzi wa masuala ya wazee tu, ili kuwaondoshea usumbufu wazee wengi wanaotibiwa kwa kuondoshwa njiani tu bila ya uangalizi wa kina kwa mujibu wa hali zao.

Aidha, waliiomba Serikali kupitia vyuo vya Afya nchini kuona umuhimu wa kuongezwa kufundishwa kozi maalumu ya kada ya utaalamu wa kuwatibu na kuwashuighulikia wazee na iwe endelevu kwa manufaa ya wazee wa sasa na wabaadae.

Pamoja na kuangalia upya kada ya uzazi ambayo alieleza vyuoni inafundishwa kwa kiwango kidogo sana, hivyo aliziomba mamlaka husika kuona haja ya kuongezewa muda ili kuepusha changamoto zinazowakabili mama wajawazito kwa uchache wa wataalamu.

Pia Katibu huyo aliiomba Serikali kupitia mamlaka husika kuangalia uwezekano wa wazee kuwekwa kwenye mfumo wa mpya wa Afya ambao utawatambua rasmi Wazee, wanawake na watoto ili kuwaepushia kuwakosesha haki zao za msingi ambapo walilaumu kwamba kuna baadhi ya mifumo ya afya haiwatambui wazee hao.

Hata hivyo, wazee hao walimshukuru Dk. Mwinyi kwa uamuzi wake wakuwaongezea pencheni na pencheni Jamii kutoka kima cha chini hadi asilimia 100 na 150 kwa pencheni jamii na wastaafu.

Kwa mujibu wa Jumuiya ya Wazee na Wastaafu, Zanzibar (JUWAZA), ilianzishwa wakati wa awamu ya tano ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mwaka 2016 ilianzishwa pencheni jamii. Wazee wote tangu mwaka 1960 ni 57,000 na wazee wa penche ni 28,000 kwa mujibu wa jumuiya hiyo.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu