AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


DK. MWINYI AISHUKURU MAREKANI KUSAIDIA SEKTA YA AFYA NCHINI

alternative

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutambua umuhimu wa ushirikiano ili kufikia malengo kwa kuwekeza rasilimali fedha katika  kuimarisha utafiti, kuboresha miundombinu ya afya, na kuhakikisha upatikanaji matibabu sawa kwa  wagonjwa wa saratani nchini.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika jukwaa la uwekezaji linalolenga kuimarisha huduma za saratani nchini, ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam tarehe:06 Februari 2024.

Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa kupitia ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, watafiti na wataalamu wa tiba kunaweza kubadilisha taswira za huduma za matibabu ya saratani nchini.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani kwa kujenga miundombinu ya huduma za afya, mikakati ya upatikanaji wa huduma bora za matibabu bora kwa wote.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya Marekani kwa ushirikiano wao kufanikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya nchini.

Pia amewashukuru wadau wa Global Health Catalyst  ambao wamejitolea kushirikiana na Serikali katika mapambano ya maradhi ya saratani, wawekezaji wa ndani wakiongozwa na Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) pamoja na  CEO Roundtable kwa utayari walionyesha kushirikiana na Serikali. 

Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uongozi na jitihada zake za kuimarisha ustawi wa maendeleo nchini

alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu