AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


WAZEE WA CCM WATOA NENO KWA DK. MWINYI

alternative

BARAZA la wazee la Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar limempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kupandisha pensheni kwa wastaafu kwa asilimia 100 ambapo utaratibu huo mpya unatarajia kuanza ifikapo Julai mwaka mpya wa bajeti utakapoanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisini kwao Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui mjini Unguja Mwenyekiti wa Baraza hilo Khadija Jabir Mohamed alisema Baraza la wazee limepokea taarifa hiyo kwa furaha kubwa kwa kuona kuwa bado Rais Dk.Mwinyi anaendeleza azma na malengo ya mapinduziya kuhakikisha wazee wanatunzwa.

"Kama mnavyokumbuka katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku za wafanyakazi zilizofanyika viwanja vya skuli ya Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo Rais Dk.Mwinyi alikuwa mgeni rasmi na aliahaidi kupandisha pensheni kwa wastaafu kwa wastaafu wa kima cha chini kufikia sh.180,000 kutoka sh.90,000 hii kwetu ni tunajivunia sana,"alisema

Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo alisema mbali na hilo pia Baraza la wazee linampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kupandisha pensheni jamii kwa asilimia 150 kwa wazee kuanzia miaka 70 ambapo wanatarajia kupokea sh.50000 kutoka sh.20000 ambayo wanayopokea hivi sasa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CCM Zanzibar Haji Machano Haji alisema hatua hiyo iliyofanywa na Rais Dk.Mwinyi ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambapo katika ibara ya 214 inaeleza kuwa CCM inatambua umuhimu wa wazee katika Taifa letu na itaendeleakuwapatia huduma za kijamii na kisheria.

"Kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ibara 214 CCM inaielekeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kipindi cha miaka mitano ijayo Kutekeleza mpango wa pensheni jamii kwa wazee wenye umri wamiaka 70 na kuendelea kwa kuongeza bajeti ya mpango kutokash.bilioni 6.5 hadi sh.bilioni 7 kwa ajili ya malipo ya wazeewalioongezeka Unguja na Pemba,"alisema

Katibu huyo alisema ikiwa Baraza hilo la wazee ni miongoni mwa wazee ambao wananufaika na pensheni hiyo wazee hao wanampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa uamuzi huu wa kuongeza kiasi hicho cha pesa kwa wazee na kwamba bado baraza hilo lina imani naye kubwa kwa kuwatunza wazee wa Zanzibar.
 

Albamu