NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amewasihi Wananchi wa Jimbo la Kwahani kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM kwani ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa vitendo.
Nasaha hizo amezitoa wakati akizindua kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo katika Uwanja wa Tawi la CCM Sebleni Zanzibar.
Alisema CCM imejipanga kuhakikisha mgombea wake anashinda katika Uchaguzi huo ili kuendeleza maendeleo na ustawi wa jamii katika Jimbo hilo ambalo ni ngome ya CCM toka kuanzishwa kwa mfumo wa Vyama vingi vya siasa nchini.
Katika maelezo yake Dkt.Dimwa,amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi amefanya kazi kubwa na nzuri,hivyo anastahili kupewa Viongozi imara na makini wanaotokana na CCM ili wamsaidie kazi.
" Maendeleo ya Jimbo hili yatazidi kuimarika zaidi chini ya Viongozi wachapakazi,waadilifu na wachapakazi wanaojali utu na maisha ya Wananchi wote bila ubaguzi wa kisiasa,kikabila na kidini na kazi hiyo ataifanya kwa ufanisi mkubwa ndugu yetu Khamis Pele." alisisitiza Dkt.Dimwa.
Akizungumzia mafanikio ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 uliofanyika katika Jimbo la Kwahani ikiwemo ujenzi wa Skuli ya kisasa ya ghorofa Shehia ya Muungano iliyogharimu zaidi ya Bilioni 6.1,ujenzi wa Soko la Kwahani uliogharimu kiasi cha zaidi ya milioni 500, wanufaika wa miradi wa TASAF ni 242 unaogharimu zaidi ya milioni 577.4 pamoja na utoaji wa Pencheni Jamii kwa Wazee 582.
Pia utekeleza wa Ilani ya CCM kwa upande wa Mbunge na Mwakilishi wameimarisha sekta za Elimu,afya,maji safi na Salama, ujenzi wa Ofisi za CCM ngazi zote,vikundi vya ujasirimali, ununuzi wa vifaa vya michezo na misaada ya Kijamii kwa Wananchi vilivyogharimu shilingi 467.8.
Kupitia Mkutano huo Dkt.Dimwa, alimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea huyo Khamis Yussuf Mussa (Pele), na kumsisitiza kuwa ilani hiyo ndio mkataba kati ya wananchi na CCM hivyo akishinda kazi kubwa ya kuendeleza maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.
Kampeni hizo za Uchaguzi huo zinafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ahmada Yahya Abdul Wakil (Shaa) tarehe 8,April 2024 kwa maradhi ya shinikizo la damu, na Uchaguzi huo umepangwa kufanyika June 8, mwaka 2024.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
09-01-2026
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
09-01-2026
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
09-01-2026
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
09-01-2026
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
09-01-2026
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
09-01-2026
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
09-01-2026
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
09-01-2026
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
09-01-2026
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
09-01-2026