Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman amesema Serikali haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi unaoendelea wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi jambo ambalo linarejesha nyuma dhamira ya Dkt. Hussein Mwinyi ya kuondoa changamoto zote za Elimu kwa wanafuzi wa Mikoa yote ya Zanzibar.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa skuli ya Sekondari ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuitembelea skuli hio kila ifikipo mwisho wa mwezi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali imeshailipa Kampuni ya Fuchs Contraction Limited shiling Bilioni 4.08 ili kuharakisha umalizikaji wa Ujenzi wa Skuli hiyo lakini kasi ya ujenzi bado inasuasua na kupelekea wanafunzi kuendelea kufuata huduma ya elimu maeneo ya mbali na makaazi yao.
Amesema kuwa endapo Mkandarasi kutoka kampuni ya Fuchs atashindwa kumaliza ujenzi wa skuli hio na nyenginezo amabazo zinajengwa na kampuni hio kwa wakati ambao wamekubaliana katika mkataba wao itakuwa wamejinyima fursa ya kufanya kazi ndani ya Zanzibar hasa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nane(8) na serikali haitalifumbia macho jambo hili.
Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Nane(8) inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Ali Mwinyi ni kuondoa changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na kuwekeza zaidi katika Sekta ya elimu ambayo ndio muhimili mkuu wa maendeleo nchini.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefika katika skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la dahalia ya wanawake liloungua moto na kusababisha hasara kubwa kwa wanfunzi wanaosoma skulini hapo, na kuwataka walimu na wanafunzi kuendelea kulitunza na kudumisha usafi ndani na nje ya jengo hilo ili liweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mhe. Hemed ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Elimu kuhakikisha ndani ya muda mfupi ujao wanaijengea uzio skuli hio ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanafunzi wanaishi hapo sambamba na kumtaka Mkandarasi kutoka Kampuni ya Faster kuhakikisha anamalizia matengenezo madogo madogo yaliyobakia ndani ya siku tano(5) ili wanafunzi waweze kuhamia na kuendelea na masomo yao katika hali ya utulivu.
Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulghulam Hussein amesema wizara imejipanga kuhakikisha inaipatia kila skuli vifaa vya kusomea vya kisasa ili kuboresha mfumo wa elimu Visiwani ZanzibarambapoWizara imefanya ununuzi wa vifaa mbali mbali ikiwemo vitanda zaidi ya elfu moja(1000) kwa ajili ya skuli ambazo zinamadahalia Kompyuta, Projecta, viti na meza ambavyo vyote vitagawiwa kwa skuli zote za Unguja na Pemba.
Mhe. Gulam ameiomba Serikali kuichukulia hatua ya kuipiga penalt Kampuni ya Fuchs kwa kusababisha kuchelewa kumalizika kwa Ujenzi wa Skuli nane (8) zinazojengwa na kampuni hio jambo ambalo litatoa fundisho kwa kampuni nyengine zitakazopatiwa fursa ya kufanya kazi na Serikali ya Awamu ya Nane (8).
Kwa upande wake Mkandarasi kutoka kampuni ya Fuchs Contraction Ltd Devid Mwasomola amesema changamoto kubwa iliosababisha kishindwa kuendelea na Ujenzi wa Skuli hio ni kukosekana kwa nondo na malipo kwa ajii ya wafanyakazi hivyo ameaahidi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi hio ndani ya muda uliopangwa kwa sasa.
Katika ziara hio Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametembelea ujezi wa skuli ya ghorofa (G+3) ya Sekondari ya Makunduchi inayojengwa na Kampuni Fuchs Contraction Limited, na kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la dahalia ya wanawake katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame liloungua moto na kusababisha athari kubwa kwa wanafunzi wanaoishi hapo mwishoni mwa mwaka jana.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
08-11-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
08-11-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
08-11-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
08-11-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
08-11-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
08-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
08-11-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
08-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
08-11-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
08-11-2025