AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


CCM TUMEIMARIKA ZAIDI - DK. DIMWA

alternative

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)Zanzibar kimewataka watendaji wake kujiimarisha na mabadiliko ya mienendo ya hali ya siasa inavyokwenda.

Akizungumza katika ziara ya sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM,Zanzibar mkoa wa Kaskazini Unguja,Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa'.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema CCM pamoja na jumuiya zake zinapaswa kujithatiti,kujijenga na kujijenga kuwa na uwezo mpya wa kulingana na uzito wa mapambano ya kisiasa yaliyopo.

"Siasa zetu zimeanza kubadilika sana na wala si siasa za kwenye majukwaa hivi karibuni juzi ACT-Wazalendo walisema tunamsubiri Dk.Dimwa ajibu hoja nasema tutajibu hoja kwa hoja tena tuna joja nyingi za kujibu," alisema

Alisema katika hilo hoja hizo haitaitoa kwenye reli CCM katika kutekeleza ilani ya uchaguzi.

"Wanazungumza suala la ujenzi wa uwanja wa Amani kuwa fedha zinazotoka wapi bila ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi lakini wawakilishi watakuwa wanajua kuwa kuna mfuko wa serikali ambao unaitwa mfuko wa hazina ndio kazi yake hii,"alisema

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema yeye ana uzoefu wa suala hilo kutokana na kuwa ameshawahi kuwa Mwakilishi kwa hivyo anatambua jambo hilo na kwamba atawajibu hoja kwa hoja na si kujibu mambo mengine.

Alisema CCM itaendelea kuhubiri amani ili Zanzibar iendelee kubaki na amani na kuachana na maneno ya wapinzani yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Pia,alisema, vyama vya siasa muda wote vinatakiwa kuhubiri amani kutokana na kuwa ikitoweka haiwezi kurudi tena, na kwamba CCM itaendelea kuhubiri amani.

"Licha ya kuwa vyama vyengine vya siasa vimekuwa vikihubiri uvunjifu wa amani lakini sisi hatutahubiri masuala hayo na tutaendeleza amani ya nchi iliyopo ili tuweze kupeleka maendeleo kwa wananchi wote bila ya kubagua," alisema.

Alisema CCM itaendelea kujibu hoja kwa hoja ambazo serikali inayoongozwa na CCM imefanya maendeleo ikiwemo, kujenga shule za kisasa za ghorofa.

Mbali na hilo,Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka viongozi wa CCM kuendelea kutangaza maendeleo yanayofanyika kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM inavyotekelezeka kwa wananchi.

"Tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele, awahamasishe wanaCCM kuyatangaza mafanikio yanayotekelezwa chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi,"alisema

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu