AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


DK.MWINYI  AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA QATAR  KUJA ZANZIBAR

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi  baada ya kuwasili jana usiku jijini Doha, Qatar  akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi utakaofunguliwa kesho.

Katika ziara yake Rais Dk. Mwinyi leo asubuhi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Qatar Mhe. Muhamed Bin Ahmed Al-Kuwari na  wadau kutoka sekta binafsi ya Viwanda.

Dk. Mwinyi aliwakaribisha wafanyabiashara hao wakubwa kuwekeza zanzibar kutokana na fursa zilizopo pia aligusia eneo jipya la uwekezaji ambalo ni utalii wa kumbi za mikutano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA Shariff Ali Shariff alieleza umuhimu wa kukutana kwa Mabaraza ya uwekezaji ya Zanzibar na Qatar ili kuimarisha uhusiano zaidi.

Pia alielezea fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar  zaidi kwa upande wa utalii kwani ujenzi wa hoteli kubwa za kifahari unahitajika kutokana na soko la utalii kuongezeka.

Fursa nyingine alizowakaribisha kuwekeza ni ukodishaji wa visiwa vidogo.

Halikadhalika aliwafahamisha kwa undani fursa zilizopo katika sera ya uchumi wa Buluu ambayo imewagusa zaidi wawekezaji hao hasa suala la uchimbaji wa gesi na mafuta.

Eneo jingine ni shamba la Makurunge Bagamoyo ambalo ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar linalofaa kwa utalii na hata kilimo.

 

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu