Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameitaka Kampuni ya Fuchs Contraction Ltd ambayo imepewa dhamana ya kujenga skuli nane (8) za Gorofa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo ndani ya muda uliopangwa na kiwango kilichokusudiwa ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri
Ameyasema hayo katika ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa skuli zinazojengwa na Kampuni hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo.
Mhe. Hemed amemuagiza Mkandarasi wa majengo hayo kuongeza nguvu kazi na kufanya kazi mchana na usiku ili kuhakikisha Miradi hio inakamilika kwa wakati na kiwango kilichokusudiwa ili kuwaondolea changamoto wanafunzi ya kufata elimu masafa ya mbali jambo ambalo linapunguza umakini na ufaulu kwa wanafunzi hao.
Amesema mtazamo na adhma ya Rais Dkt Hussen Mwinyi ni kujenga skuli za kisasa zenye viwango na zenye kuendana na wakati sambamba na kuweka vifaa vya kutosha vya kufundishiia ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani pamoja na kuingia mkondo moja tu kwa wanafunzi wote wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila aina ya ushirikiano kwa wakandarasi hao na kuwahakikishia kuwa kiwango cha fedha kilichobakia kitalipwa ndani ya siku chache zijazo ili kuharakisha umalizikaji wa ujenzi huo na wanafunzi waliopangishwa katika maskuli jirani waweze kurejea maskuli mwao.
Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulghulam Hussein amesema ziara ya kutembelea Miradi ya Ujenzi wa Skuli za gorofa zinazoendelea kujengwa itatoa matokeo chanya ndani ya muda mfupi ujao na uongozi wa wizara utahakikisha majengo yote yanamalizika kwa kiwango cha hali ya juu.
Naibu Waziri Ghulam amesema vifaa vyote kwa ajili ya maskuli yanayojengwa Zanzibar vipo tayari na Wizara imetenga Bajeti kwa ajili ya kuyafanyia ukarabati mkubwa maskuli yote yaliyoanza kuchakaa ili yaendane na hadhi ya majengo yanayojengwa sasa.
Kwa upande wake Mwakalishi wa mmiliki wa Kampuni ya Fuchs Contraction Ltd Ndugu YASIN FEISAL IBRAHIM amesema Kampuni imejipanga kufanya kazi usiku na mchana na kuahidi kukamilisha ujenzi wa maskuli hayo kwa ubora na viwango vya hali ya juu ifikapo mwishoni mwa mwezi wa nane(8).
Mkandarasi Feisal amesema kulikuwa na changamoto ndogo ndogo ambazo zilikwamisha ujenzi huo lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa hivyo watahakikisha wanapambana ili waweze kukabidhi kwa wakati na kutumia fursa hio kuiomba Serikali kuwamalizia malipo ya fedha zilozobaki ili kazi iendelee kwa haraka zaidi.
Mapema Mshauri elekezi kutoka wakala wa majengo Zanzibar (ZBA) MOH'D NAHODA MOH'D amesema makubaliano ya awali na Kampuni ya Fuchs ni kukamilisha Ujenzi huo mwishoni mwa mwezi wa saba(7) lakini imekuwa tofauti na ujenzi huo unaonekana kusuasua jambo ambalo linachelewesha mipango ya Serikali ya kuboresha miundombinu ya Sekta ya Elimu kama ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoelekeza.
Mkandarasi Nahoda amesema endapo kampuni ya Fuchs itashindwa kukamilisha kwa wakati miradi hio ZBA kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali watangali ni kwa namna gani wanaweza kufanya maamuzi ya kisheria dhidi ya kampuni hio ili kuwaweka sawa wakandarasi wengine waliopewa dhamana ya kujenga miradi ya Serikali.
Katika ziara hio makamu wa pili wa rais wa Zanzibar ametembelea ujenzi wa skuli za ghorofa ikiwemo CHUMBUNI, MAUNGANI, MWERA, REGEZAMWENDO, KIJICHI, CHUMBUNI na MUUNGANO.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
06-11-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
06-11-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
06-11-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
06-11-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
06-11-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
06-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
06-11-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
06-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
06-11-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
06-11-2025