Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema ujio wa nyota maarufu wa filamu nchini China, Jin Dong, utaendelea kuifungulia Zanzibar soko la Utalii kutoka China.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema ujio wa nyota maarufu wa filamu nchini China, Jin Dong, utaendelea kuifungulia Zanzibar soko la Utalii kutoka China.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipotembelewa na msanii huyo ambaye yupo Zanzibar kwa kazi ya kutengeneza filamu.
Alisema, ujio wake ni fursa adhimu kwa Zanzibar kutangazwa kimataifa hasa kupitia Sekta ya Utalii ambayo ni Sekta mama ya uchumi wa Taifa.
Rais Dk. Mwinyi alimueleza mgeni wake huyo, kwamba Zanzibar ina vivutio vingi vya Utalii, ukiwemo Utalii wa fukwe safi nyeupe zinazovutia wengi duniani, Utalii wa utamaduni, Utalii wa Mji mkongwe, Utalii wa michezo, Utalii wa visiwa pamoja na wa Mikutano.
Aidha, alimkaribisha mgeni huyo kuitumia fursa ya kuwepo kwake Zanzibar kutembelea maeneo muhimu ya Utalii likiwemo shamba la viungo vya Zanzibar, Kisiwa cha Mnemba, Kaskazini Unguja pamoja na Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Naye, nyota huyo wa Filamu nchini China, Jin Dong, alimueleza Rais Dk. Mwinyi furaha yake ya kufika Afrika kwa mara ya kwanza tena ndani ya visiwa vya Zanzibar kwa nchi za Afrika Mashariki.
Alisema, mbali na Safari ya Sanaa hapa Zanzibar lakini pia ujio wake unaimarisha uhusiano wa undugu na urafiki uliopo baina ya China na Tanzania ikiwemo Zanzibar.
Aliahidi kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Zanzibar kwa Utalii na alieleza imani yake ya kuwavutia Wachina wengi kuja kutalii visiwa vya Zanzibar.
Miongoni mwa maeneo ya Utalii aliyotembezwa msanii huyo ni kisiwa cha Mnemba, Mji Mkongwe maeneo ya Forodhani na Ngome Kongwe.
Jin Dong ni nyota mkubwa China mwenye wafuasi wa mitandao ya kijamii zaidi ya milioni 15. Mbali na kazi za Sanaa pia ni Mwanasiasa nai Naibu Mkurugenzi wa kikundi cha Sanaa cha serikali cha utamaduni.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
23-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
23-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
23-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
23-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
23-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
23-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
23-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
23-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
23-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
23-12-2025