CCM ZANZIBAR YAIPONGEZA ZIPA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kimeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika eneo la uwekezaji kupitia Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar(ZIPA).
Kauli hiyo ameitoa jana Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji ZIPA,Shariff Ali Shariff ofisini kwake Maruhubi.
Alisema ZIPA imetekeleza kwa kiasi kikubwa azma ya Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ya kuwavutia wawekezaji ambapo miradi mingi tayari imekwishawekezwa kwa kipindi kifupi.
"Eneo la uwekezaji ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar hivyo niwapongeze ZIPA kwa kazi nzuri mnayoifanya na kasi kubwa mnayoitekeleza ya ilani ya chama chetu," alisema.
Katibu huyo aliitaka ZIPA kuendelea kufanya kazi kwa karibu na CCM ili kufikia malengo ya ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo wazanzibari.
Naye, Mkurugenzi wa ZIPA Sharif Ali Sharif, alisema, mwekezaji anapotaka kuwekeza anapewa masharti kwa kuhakikisha anazingatia mazingira ya uwekezaji yenyewe.
Alisema kwa sasa ZIPA imekuwa na uwekezaji wa miradi mikubwa 226 ambayo inaweza kuzalisha dola za kimarekani bilioni 3.5 ambapo inatengeneza ajira zaidi ya 13000.
"Katika kipindi cha miaka hii miwili ya serikali ya awamu ya nane ZIPA kupitia serikali tumetekeleza ilani kwa vitendo jambo ambalo imeonyesha dhamira kwa serikali kuhakikisha uchumi unaongezeka,"alisema
Alisema katika kipindi cha miaka miwili wawekezaji wameongezeka kutokana na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Rais, Dk. Mwinyi kutokana na kuwa ametengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji.
"Rais Dk.Mwinyi ameiimarisha ZIPA kiutendaji kwani Mamlaka hii imekuwa na watendaji wenye uwezo mkubwa wa kitaalamu katika kuwavutia wawekezaji na pia wameweka sheria ambayo ni rafiki zaidi kwa wawekezaji,"alisema
Alisema kupitia miradi hiyo zimepatikana ajira mbalimbali kwa wananchi wa Zanzibar na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha uchumi wa unaongezeka kwa asilimia kubwa.
Pia, alisema uwekezaji umeongezeka kutokana na serikali kuanzisha kituo cha pamoja ambacho kinatoa huduma zote kwa wakati mmoja ambapo wawekezaji wamekuwa wakirahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wakati.
Akizungumzia upande wa visiwa, Mkurugenzi Sharif, alisema, kibali kinachotolewa kwa muwekezaji hupewa masharti ya asilimia 10 ya eneo husika na asilimia iliyobakia hupewa masharti ya kujenga ndani ya eneo la baharini ili kuona visiwa hivyo havihathiriki na uwekezaji huo.
Mkurugenzi huyo alisema katika uwekezaji huo,muwekezaji utanguliza fedha kabla ya kuwekeza ambapo kwa sasa serikali imeshaingiza dola za kimarekani milioni 14 ambapo katika miradi ya visiwa hivyo inatakiwa kuingiza dola za kimarekani milioni 19.
"Wawekezaji hawa wamekuwa wakilipa kwa awamu na fedha zilizoingia zipo na zitatumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kulipwa fidia watu waliokuwepo katika bahari ikiwemo wavuvi, na wawekezaji ambao hawakufikia vigezo tunavyovitaka," alisema
Akizungumzia suala la viwanda ndani ya visiwa vidogo alisema, katika uwekezaji huo kutotakiwa uwekezaji wa viwanda vikubwa na kwamba viwanda vinavyotakiwa ni vya kati na vyepesi ambavyo vitakuwa na thamani kubwa.
Mbali na hilo,alisema ZIPA itaendelea kutekeleza ilani ya CCM katika utendaji wao wa kazi wa kila siku na kufuata miongozo ya Rais Dk.Mwinyi juu ya uwekezaji nchini.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
16-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
16-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
16-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
16-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
16-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
16-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
16-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
16-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
16-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
16-12-2025