MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DK. HUSSEIN ALI MWINYI AMEKUTANA NA SEKRETARIETI ZA MIKOA NA WILAYA
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na sekretarieti ya kamati maalum, sekretarieti za Mikoa na Wilaya CCM Zanzibar katika kikao chake cha kwanza na watendaji hao ukumbi wa Afisi kuu CCM Kisiwandui tarehe: 5 Februari 2024.
Aidha, Makamu Mwenyekiti CCM Dk.Mwinyi amesema kazi kuu ya Chama cha siasa ni kushinda chaguzi za dola.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Mwinyi amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vema Chama cha Mapinduzi na kukiimarisha.
Kwa upande mwingine Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi amewapongeza watendaji kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuimarisha chama na kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Halikadhalika Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi amewataka watendaji kutoa fursa sawa kwa wagombea wote na kujiepusha kutengeneza makundi wakati wa uchaguzi.
Vilevile amewasisitiza watendaji hao wana wajibu wa kusimamia kanuni za chama kuhakikisha umoja , amani na utulivu una kuwepo ndani ya chama.
Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi amewataka wana CCM wote kuwa mstari wa mbele kuelezea vema mafanikio ya ilani ya utekelezaji wa CCM kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa kugusa sekta nyingi za utekelezaji pamoja na kuvuka lengo ikiwemo sekta elimu, afya , barabara, maji, uwezeshaji wa vikundi vya wajasiriamali n.k
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
22-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
22-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
22-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
22-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
22-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
22-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
22-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
22-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
22-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
22-12-2025