AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


Serikali itaendelea kuweka mazingira Bora kwa Taasisi na Mashirika binafsi katika kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria haapa -nchini.

alternative

Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika kilele cha maadhimisho ya Tano(5) ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar yaliyofanyika katika Ukumbi wa asheikh aidrisa Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar.

Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali kwa kushirikiana na Idara ya Katiba na Sheria itaendelea kutekeleza kampeni Kitaifa ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia na Kampeni  nyenginezo za Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kuwawezesha wananchi katika suala la upatikanaji wa haki zao.

Aidha Dkt Mwinyi amesema watoa huduma za msaada wa Kisheria wamekuwa wakombozi wakubwa kwa jamii katika masuala ya kisheria, kwa kutoa elimu ya kisheria na msaada wa kisheria kwa makundi mbali mbali wakiwemo vijana, wazee, watu wenye Ulemavu na wanafunzi ambapo wameweza kuwafikia wananchi  laki nne kumi na tisa elfu mia nne na moja ( 419, 401) kati yao wanawake ni laki mbili ishirini na sita elfu mia moja na sabiini na mbili ( 226, 172) ni wanawake na laki moja tisiini na tatu mia mbili na ishirini na tisa (193, 229) ni wanaume.

Sambamba na hayo Rais Dkt Mwinyi amesema uwepo wa namba maalum itakayowasaidia wananchi katika upatikanaji wa huduma za Msaada wa Kisheria ni hatua muhimu inayohamasisha upatikanaji wa huduma hio na itakuwa kiungo kikubwa baina ya watoa huduma za Msaada wa Kisheria na wananchi ambao wengi wao mjini na vijijini wanamiliki vifaa vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi.

Rais Dkt Mwinyi ametoa wito kwa Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria pamoja na watoa huduma za Msaada wa Kisheria kuendelea kuelimisha wananchi juu ya uwepo wa namba hio maalum ya Huduma za Msaada wa Kisheria pamoja na upatikanaji wa huduma hizo kwa njia ya Teknolojia na kuwataka wananchi kuitumia vyema namba hio kwa utaratibu uliowekwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema watoa Msaada wa Kisheria wanafanya kazi kubwa ya kujitolea katika kutoa elimu ya Sheria na Msaada wa kisheria kwa wananchi hivyo ameiomba Serikali kuangalia ni kwa namna gani itawasaidia watoa huduma hao  katika kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Waziri Haroon amesema ili kuendelea kuisaidia jamii katika kuwapatia elimu na kutoa Msaada wa Kisheria ni lazima kuwepo na mazingira mazuri ya kufanyia kazi, hivyo amewaomba Wakuu wa Mikoa na Wilaya  kuwapatia ofisi watoaji wa Msaada wa kisheria katika kila Wilaya ili waweze kutekeleza majukumu yao  kwa utulivu na kwa ufanisi mkubwa.

Kwa upande wao wawakilishi wa mashirika ya msaada wakisheria wakiwemo UNDP, LSF na UN WEMEN wamesema wataendela kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  na wadau mbali mbali katika kupambana ili kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wahanga wa vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia hasa wanawake na watoto uanpatikana kwa wakati.

Wamesema kusaidia na kupambana kwa hali zote  katika harakati mbali mbali za kimaendelo hasa katika kuhakikisha upatikanaji wa haki,  haki za Binaadamu zinalindwa na kuhakikisha  elimu ya Sheria inawafikia wananchi wote mijini na vijini.

Mapema  Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Bi. Hanifa Ramadhan Said  amesema Idara ya Katiba imeona ipo haja ya kuanzisha namba maalum ambayo itatumika katika kurahisisha upatikanaji wa Msaada wa kisheria na kuwa kiunganishi kikubwa kati wa Idara , watoa huduma za Msaada wa Kisheria na wananchi.

Mkurugenzi Hanifa amesema Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria itahakikisha inazidisha ushirikiano katika utendaji wa kazi baina yao na watoa huduma za Msaada wa Kisheria ili lengo halisi la upatikanaji wa haki, kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi liweze kufikiwa .

Amezishukuru Taasisi na Mashirika mbali mbali ikiwemo L.S.F, UNDP, UN WOMEN Mahakama, Polisi na Chuo cha Mafunzo kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoendelea kuwapatia ambao unarahisisha katika harakati zao za  ufanyaji wa kazi za kila siku.

Nao watoaji Msaada wa kisheria Wameishukuru Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria kwa kuwapatia ushirikiano mkubwa unaowapelekea kufanya kazi zao za uweledi na ufanisi mkubwa sambamba na kuiomba serikali za mikoa na wilaya kuwapatia ofisi  za kufanyia kazi zao ili kufikia malengo waliojiwekea.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu