AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA NA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA MHE. ELIZABETH JACOBSEN IKULU ZANZIBAR

alternative

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali ya Norway kwa jitihida zake za kuendelea kuiunga mkono Tanznia ikiwemo Zanzibar kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.

Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elizabeth Jacobsen aliyefika kuaga baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi nchini.

Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi Jacobsen kwamba, Zanzibar imenufaika na fursa nyingi kutoka Norway zikiwemo sekta za Afya, Umeme na Elimu.

Amesema uhusiano wa Norway na Tanzania utakumbukwa zaidi kwa kuinufaisha Zanzibar kupitia sekta ya umeme, hasa wa kutoka Tanga hadi Pemba na Dar es Salaam hadi Zanzibar ambapo Dk. Mwinyi alieleza, Norway ilitoa mchango mkubwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaznia katika kuwafikishia huduma bora wananchi.

“Tunaishukuru Serikali ya Norway kwa kuendelea kutuunga mkono Tanzania, hasa kwenye sekta za Afya na umeme, tunashukuru Norway imetuungamkono kwenye sekta ya umeme, ilisaidia kueneza umeme visiwani Zanzibar” alisifu Rais Dk. Mwinyi.

Aidha, Dk. Mwinyi alimueleza balozi huyo dhamira ya Zanzibar kutaka kujitegemea kwa umeme wake wenyewe ili kuwapatia huduma ya uhakika wananchi wa Unguja na Pemba badala ya kutegemea umeme kutoka Tanzania Bara.

“Kwa hatua tuliofikia sasa, Zanzibar inataka isimame wenyewe ijitegemee wenyewe umeme wake utakaozalishwa hapa hapa Zanzibar” alieleza Dk. Mwinyi.

Pia alisifu Rais Dk. Mwinyi, alisifu ushirikiano ulipo baina ya Norway na Tanzania hasa kwenye nyanja za afya na elimu na kueleza Serikali ya Norway imetoa mchango mkubwa kwa Tanzania kwa kuwajengea uwezo Watanzania wengi kupitia vyuo vikuu vya nchi hiyo.

“Hatunabudi kuishukuru Serikali ya Norway, kupitia vyuo vikuu vya afya vya huko vimewajengea uwezo watu wetu kupitia sekta za Umma na binafsi” alisifu Dk. Mwinyi.

Akizungumza na Rais Dk. Mwinyi, Balozi Elizabeth ameisifu Tanzania kuendelea kuwa nchi ya amani, yenye raia wenye upendo, ushirikiano, umoja na utulivu wa kisiasa akieleza kuwa Tanzania ni kielelezo cha nchi ya mfano barani Afrika na kwengineko duniani kuwa ni taifa lenye demokrasia kwa kutekeleza na haki za binaadamu na siasa safi.

Balozi huyo alimuahidi Rais Dk. Mwinyi, kwamba Serikali ya Norway daima itaendelea kuiungamkono Tanzania ikiwemo Zanzibar kwenye sekta za Maendeleo.

Alisema Serikali ya Norway inajivunia uhusiano wa muda mrefu wa diplomasia uliopo baina yake na Tanzania na kusifu zaidi ya miaka 50 yaushirikiano wao kwenye masuala mbalimbali iliwemo ushirikiano walionao baina ya vyuo vikuu vya Norway na Tanzania ni chachu iliyokuza urafiki baina ya watu wa mataifa wawili hayo kwenye nyanja mbalimbali za jamii na uchumi.

alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu