AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


Wazazi na walezi wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kupata kizazi chenye hofu ya Allah kitakachosaidia kuziondosha changamoto zilizopo zinazosababishwa na kukosekana kwa maadili mema kwa vijana.

alternative

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid JAMII WATHABATUL- KHEIR iliyopo KOANI kwa KOZI Wilaya ya Kati  mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

 

Amesema ni wajibu wa kila mzazi na mlezi  kuwalea watoto wao katika maadili  mema yatakayowajenga kidini na kiimani jambo ambalo litasaidia Taifa kupata viongozi bora wa baadae na wenye kufanya kazi zao kwa hofu ya Mwenyezi Mungu.

 

Alhajj Hemed amesema wakati umefika wa jamii kujitathmini katika malezi wanayowalea watoto wao ili kupunguza malalamiko ya mmong’onyoko wa maadili unaopelekea vijana kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo udhalilishaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Sambamba na hayo Alhajj Hemed ameendelea kuwasisitiza  wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla kuzidi kudumisha Amani na Utulivu uliopo nchini jambo ambalo huwaweka huru katika kufanya shuhuli zao mbali mbali za kujitafutia maisha kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Sheikh SALIM MASSOUD SEIF  amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuendelea kuzilea vyema familia zao ili kuweza kupata watoto wema ambao watakuwa wema sasa na hadi kuondoka kwao duniani.

Amesema kuwa waislamu ni lazima kushirikiana na kuamrishana mambo mema na kukatazana mabaya ili kujikurubisha karibu na Allah (S.W) na kufikia lengo la kuumbwa mwandamu hapa duniani

alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu