SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inahitaji uwekezaji mkubwa katika sekta ya Maji na Umeme ili kuongeza ufanisi wa hali ya juu wa huduma ya uhakika kwenye sekta hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na uongozi wa Kampuni ya “WAPCOS Limited” ya nchini India, uliofika Ikulu Zanzibar.
Dk. Mwinyi amesema hadi sasa Zanzibar inapokea megawati 110 za nishati ya umeme, ambao pia inapata msaada kutoka Tanzania Bara, hivyo alisema, Serikali inadhamira ya kuzalisha umeme wake mwenyewe na iko tayari kushirikiana na kampuni yoyote itakayokuwa tayari ili kuanza hatua za upembuzi yakinifu.
Pia, Rais Dk. Mwinyi amesema Zanzibar inahitaji utafiti wa kina wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa nishati hizo kwa kuangalia zaidi uwekezaji na huduma za uhakika.
Dk. Mwinyi ameikaribisha kampuni ya “WAPCOS Limited” endapo inavutika kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakaribishwa.
Alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya India ni wadau wakubwa kwenye huduma za jamii na imekua ikishirikiana kwenye nyanja mablimbali za Maendeleo ikiwemo elimu.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya “WAPCOS Limited, Rajni Kant Agrawal amesema kampuni yao imejika zaidi na kutoa huduma za ushauri hasa kwenye nishari za umeme, maji na miundombini na kueleza kuwa wako tayari kusirikiana na Serikali kwenye uwekezaji wa sekta hizo.
Alisema, kwa Tanzania tayari kampuni hiyo inafanyakazi maeneo ya Dar es Salaam, Bagamoyo na maeneo mengine ya nchi ikiwemo Zanzibar.
Kampuni ya “WAPCOS Limited” yenye makao makuu yake mjini New Delhi, India ni watoa huduma za ushauri kwa nyanja za rasilimali maji, nishati na miundombinu. Ilizinduliwa rasmi June 26, mwaka 1969, mjini New Delhi.
Ni kampuni yenye miradi kadhaa kote India, Asia na Afrika, iko chini ya umiliki wa Serikali ya India kwa usimamizi wa Wizara ya Jal Shakti nchini humo.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
08-11-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
08-11-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
08-11-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
08-11-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
08-11-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
08-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
08-11-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
08-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
08-11-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
08-11-2025