AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


KARIBUNI WANACHAMA WATAONA MIRADI MIKUBWA - DK. MWINYI

alternative

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema baada ya muda mfupi wanachama wa CCM wataona miradi mikubwa ambayo itasaidia chama kujiendesha.

Akizungumza katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mali za chama zilizopo mkoa wa Mjini na Magharibi ambapo alikagua eneo la uwanja wa Tawi la CCM Mbweni, ukumbi wa CCM Social Hall, nyumba ya CCM iliyopo Posta na eneo la Sheli la Kinazini.

Alisema nia na madhumuni ni kuimarisha mali za chama ili chama kiweze kujitegemea

"Katika ziara yangu hizi kwenye kila mkoa ninaopita tuone kwa namna gani kuna fursa zinazohusu mali zetu za chama ili tuziendeleze kwa mfano hapa tupo kwenye kiwanja wa tawi la Mbweni huu ni mradi mkubwa na kwa bahati mbaya sana haujaendelezwa na mambo mengi tungeweza kuyafanya kupitia mapato yanayopatikana,"alisema

Alisema madhumuni ya ziara yake hiyo ya kukagua mali za chama ni kutazama fursa zilizopo katika mali hizo na kwamba ana imani kuwa CCM ikishughulikia vizuri itanufaika na mapato yatakayoendesha chama bila ya matatizo yeyote.

"Natambua kuwa upo umuhimu wa maofisi zetu tusifikilie biashara tu na vile vile ofisi hizi za chama kuanzia ngazi ya mkoa,jimbo tufikirie kuwa zitakuwa wapi na za namna gani hivyo lazima ziendane na hali itakayoendana na hadhi ya chama chetu,"alisema

Katibu wa Kamati Maalum NEC, Idara ya Uchumi na Fedha CCM Zanzibar, Afadhali Taibu Afadhali,alisema alisema eneo la Mbweni lina jumla ya viwanja 10  vilivyopimwa na kupatiwa hati yenye namba Z-13/2005.

Alisema, eneo hilo lina thamani ya sh.bilion 3,138,000,000 na kwamba kwa sasa eneo hilo lina jengo la tawi la CCM Mbweni na nyumba iliyokuwa ikitumika kwa makazi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, pamoja na vibanda vya biashara.

Akizungumzia eneo la Maisara alisema, eneo hilo linamilikiwa na Ofisi kuu ya CCM kwa hati namba Z-53/s.149/117 na 118/2008 ambapo limegawika katika viwanja viwili.

Alisema, Ofisi kuu ya CCM, Zanzibar kupitia sekretarieti ya kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa Zanzibar iliridhia eneo hilo kumpa mwekezaji wa kampuni ya utalii ya Cateringi and Generel supplier ambayo ilifanya ukarabati.

Alisema, katika ukarabati huo umehusisha sehemu ya kuuzia vileo na chakula, vyumba 18 vya malazi, maduka matano, vyoo viwili, chumba maalum cha muziki pamoja na sehemu ya jiko, ambapo ukarabati huo ulifanyika kwa muda wa miezi mitano kuanzia kipindi cha Agosti mwaka 2021 hadi Januri mwaka 2022 kwa gharama ya sh. milion 485,831,820.

Katibu huyo alisema eneo la mradi wa Kijangwani ambalo lina historia kubwa kutokana ndipo ilipozaliwa Shiraz Association.

Alisema, eneo hilo limebeba historia ya chama kutokana na kuwa vikao vya sekreterieti ya Kamati maalum vilivyopita viliwahi kuazimia kulitunza kwa kujenga nyumba ya makumbusho kwa gharama ya sh.bilion 3,182,963,148.

Katika maelezo yake Katibu Afadhali alisema, lengo hilo halikufikiwa kutokana na kukosekana kwa fedha na baadaye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya saba ikaliweka katika mipango yake ya kutaka kujenga makumbusho bila ya kupoteza hadhi yake jambo ambalo hadi sasa halijafanyika.

Akitoa taarifa katika eneo la kituo cha mafuta Kinazini Katibu Afadhali alisema, ujenzi wa kituo hicho ulitokana na maelekezo ya kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa Zanzibar kukitaka Chama kuhakikisha kinaongeza mapato.

Alisema, ujenzi wa kituo hicho cha mafuta ulikamilika Oktoba 22, mwaka 2000 ambapo mgao wa ubia baina ya Chama na Mwekezaji ambaye ni Abdalla Khalfan ulianza kulipwa Juni mwaka 2001.

Albamu