AnuaniKisiwandui, Zanzibar
Simu(+255) 26 23 22965

Habari na Matukio Mbalimbali


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Ndugu.Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi kinatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na Jumuiya ya wazazi Tanzania katika kuhakikisha CCM inaendelea kushikilia dola awamu kwa awamu

alternative

Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla katika uzinduzi wa sherehe za Wiki ya wazazi Kitaifa zinazofanyika Wilaya ya Mlele  Mkoani Katavi.

Dkt Mwinyi amesema Jumuiya ya wazazi imekuwa ikifanya kazi nzuri katika kusimamia elimu, maadili na malezi bora kwa watoto yenye kufuata utamaduni wa Kitanzania jambo ambalo linaendelea kuiletea heshima kubwa Tanzania.

Amesema kuwa jumuiya ya wazazi imekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo vya ukatili, unyanyasaji na udhalishaji wa kijinsia jambo ambalo linazorotesha nguvu kazi na  maendeleo ya Taifa hivyo ni wajibu wa kila mwanajumuiya kuhakikisha anasimama imara katika kupinga vitendo hivi.

Rais Dkt. Mwinyi  amesema mtaji wa chama chochote cha siasa ni wanachama hai hivyo ameitaka Jumuiya ya Wazazi kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na CCM,  kuwapa elimu ya kupiga kura pamoja na kuwajenga kuwa na utayari wa kukipigia kura kwa wingi chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020-2025.

Aidha Makamu Mwenyekiti Mwinyi amewasisitiza viongozi kushuka chini kwa wanachama na  kufanya ziara ya kuzitembelea jumuia mbali mbali pamoja na kushika kwa wananchi kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuziwasilisha Serikali kupatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya chama na serikali.

Rais Dkt Mwinyi amesasisistiza kuwataka Watanzania kuwa Umoja na Mshikamano kwa kuweka mbele maslahi ya CCM hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu ujao ili CCM iendelee kushinda kwa kishindo na kudhikilia madaraka.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa anaefanyia kazi zake Zanzibar  Ndugu DOGO IDDI MABROUK amesema Jumiiya ya Wazazi itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha juu ya malezi bora ya watoto kwa kutambua tamaduni zao ambazo zinaonekana kutoweka na kusababisha mmong'onyoko wa maadili jambo linalopelekea kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto.

Ndugu DOGO amesema kupitia Jumuiya ya wazazi itahakikisha sera tano muhimu za jumuiya hio zinatiliwa mkazo katika utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na elimu, malezi, utamaduni, mazingira na afya ili kuhakikisha CCM inakuwa na wanachama wenye uweledi na wenye kufuata maadili kama sera na miongozi ya chama inavyoongoza.

Akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Katavi Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Mizengo Kayanza Pinda amesisitiza umoja na mshikamano kwa Watanzania wote ambao hujenga upendo miongoni mwao na kupelekea amani na utulivu ambao ndio ngao na muhimili mkubwa wa maendeleo ya Taifa.

Mhe. Pinda amewataka wanakatavi na watanzani wote kuendelea kujiandikisha katika daftari la kupigia kura ili kuweza kupata nafasi ya kukipigia kura kwa wingi chama cha Mapinduzi na kuendelea kukiweka madarakani.

Pinda amesema uhifadhi wa mazingira ni jambo la lazima kwa kila Mtanzania na kuwaomba kuacha tabia ya kukata miti na kuchoma moto kiholela misitu ya hifadhi na badala yake wajenge tabia ya kupanda miti kwa kuhifadhi mazingira.

alternative alternative
Habari Nyingine
Albamu