.DK.HUSSEIN MWINYI ASHUHUDUA ITIAJI WA SAINI YA MRADI WA SEKTA YA AFYA BAINA YA CHINA NA ZANZIBAR IKULU LEO
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali ya China kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa Tanzania ikiwemo Zanzibar kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.
Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alikoshuhudia utiaji wa shaini mikataba ya miradi mitano ya ushikirikano kwenye sekta ya afya baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Katika hafla hiyo Rais Dk. Mwinyi alisema, Zanzibar imenufaika na fursa nyingi za maendeleo kupitia misaada tofauti inayoletwa kutoka China hasa sekta za Afya na Elimu ikiwemo Tanzania kujifunza uzoefu wa masuala mbalimbali ya afya, kupokea timu za madaktari bingwa wanaofika nchini kwaajili ya kubadilishana uzoefu na wazawa hali aliyoieleza imeimarisha uhusiano mwema uliopo baina yao.
Alisema mikataba minne aliyoishuhudia sio tuu itaimarisha huduma za tiba nchini pekee, lakini itajenga ushirikiano mwema baina ya maofisa wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na China jambo alilolieleza ni ishara ya uhusiano mwema uliopo baina ya mataifa mawili hayo.
Rais Dk. Mwinyi alieleza, uhusiano wa China na Tanzania utakumbukwa zaidi kwa kuinufaisha Zanzibar kupitia sekta ya afya katika suala zima la kuimarisha miundombinu ya afya, vifaa tiba, dawa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wataalamu wa afya wazawa, pamoja na timu za madaktari bingwa wanaofika Zanzibar kila mwaka kwa nyakati tofauti na Tanzania kwa ujumla, jambo alilolieleza kwamba limeimarisha uhusiano wa China na Tanzania.
Aidha, Dk. Mwinyi alimpongeza Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar, Zhang Zhisheng kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuza ushiriiano uliopo baina ya China na Zanzibar.
“Wenzetu China mmetusaidia sana hata tukieleza hatutomaliza, nimeshuhudia utiaji wa saini mikataba minne ya ushirikiano baina ya Zanzibar na China, kupitia sekta ya afya, miradi hii itaendelea kuimarisha ushirikiano wetu uliopo” Alisifu Dk. Mwinyi.
Naye, Rais wa taasisi ya Ushirikiano baina ya Afrika na China, (CAPFA) Dk. Li Bin ameeleza miradi hiyo itatatua maradhi sugu jamii hasa kina Mama na kutoa fursa za miradi mbalimbali itakayonufaisha pande zote za ushirikiano wa Nchi hizo na kuboresha huduma za sekta ya Afya.
Dk. Li pia aliisifu Tanzania kwa ukaribu wa kihistoria baina yake na China alioueleza ni wa mda mrefu tokea uhai wa Mwenyekiti Mao Zedong na Mwl. Julius Kambarage Nyerere, zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Alisema, Tanzania imebarikiwa kuwa na raia wenye ukarimu, upendo na ushirikiano, ambao ni kielelezo chema kwenye kukuza uhusiano uliopo baina yao na China.
Alieleza, ushirikiano huo ni mwendelezo wa fikra njema za waasisi wa mataifa mawili hayo, Mwenyekiti Mao Zedong na Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kueleza Serikali ya Jamhuri ya watu wa China inajivunia uhusiano huo kwa maendeleo makubwa yaliyofikiwa na watu wa China na Tanzania ikiwemo kukuza uhusiano wa jamii na uchumi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Afya, Nassor Mazrui alisema mikataba waliyoisaini mbele ya Rais Dk. Mwinyi itagharimu dola za Marekani 4,76,000 sawa na Shilingi bilioni 1.2 za Tanzania.
Miongo mwa miradi iliyosainiwa ni pamoja na mradi wa Ushirikiano wa hospitali baina ya China na Afrika, Utafiti na udhibiti wa magonjwa ya kitropiki ikiwemo Kichocho, Uchunguzi wa saratani ya shingo ya mlango wa kizazi na kituo cha matibabu ya Mama na Mtoto pamoja na msaada wa vifaa tiba.
Aidha, hospitali zitakazonufaika na ushirikiano huo ni hospotali kuu, Mnazi Mmoja, Kivunge, Chake chake na Abdallah Mzee Pemba.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
28-12-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
28-12-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
28-12-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
28-12-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
28-12-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
28-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
28-12-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
28-12-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
28-12-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
28-12-2025