Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Wanachama wa CCM na Wazanzibari kwa ujumla wana kila sababu ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi kwa mafanikio na maendeleo makubwa aliyoiletea Zanzibar.
Ameyasema hayo katika Hafla Maalum ya Usiku wa Kumpongeza Mhe.Dkt Hussein Mwinyi kwa kutimiza Miaka minne ya mafanikio katika uongozi wake iliyofanyika katika Kiwanja cha kufurahishia watoto TIBIRINZI CHAKE CHAKE PEMBA, iliyoaandaliwa na Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Amesema katika Uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi maendeleo ya wazi yanaonekana kila kona na hakuna eneo ambalo Dkt. Mwinyi hajalifikia kimaendeleo ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais ambae pia ni Mjume wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa amewataka Wazanzibari kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Mwinyi pamoja na Serikali anayoiongoza ili kumpa nguvu zaidi ya kuendelea kuwatumikia Wazanzibari kwa mafanikio makubwa zaidi.
Aidha, Mhe. Hemed amesema Rais Dkt Mwinyi ni msikivu na mwenye kupenda umoja na mshikamano kwa wanachi wake hivyo Serikali anayoiongoza ipo tayari kupokea ushauri wenye tija utakaoileta Zanzibar maendeleo kwa maslahi mapana ya wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Sambamba na Hayo amesema Mwaka wa tano (5) wa uongozi wa Dkt Mwinyi utekelezaji wake wa maendeleo utakuwa wa kupigiwa mfano ambapo miradi mingi na mikubwa ya maendeleo itakatekelezwa kwa lengo la kuendelea kunyanyua uchumi wa wazanzibari.
Nae Katibu wa Idara ya Siasa, Itikadi, Uwenezi na Mafunzo ya CCM Zanzibar Komredi KHAMIS MBETO amesema Chama cha Mapinduzi kina kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt Mwinyi kwa mema na mazuri anayoendelea kuwafanyia wananchi wa Zanzibar.
Komred MBETO amesema wana CCM na wananchi wa Zanzibar wataendelea kumuunga mkono Dkt Mwinyi kwa dhamira yake njema ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari wote pasipo kujali rangi, kabila, dini wala jinsia zao.
Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
06-11-2025
SMZ Kuendelea kuweka Mifumo ya Kiteknolojia ya Kisasa
06-11-2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
06-11-2025
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sudan kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda.
06-11-2025
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
06-11-2025
CCM KATA YA MWANANYAMALA NA CCM MKOA WA MAGHARIB WATEMBELEA S.G.R DAR ES SAALAM-MOROGORO.
06-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amewataka mabalozi wa mashina ya CCM nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini, ufanisi, na ueledi, kwa kuhakikisha wanachama wote wenye sifa za kupiga kura wanaandikishwa katika zoezi la awamu ya pili la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwaka 2025.
06-11-2025
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), jana tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma.
06-11-2025
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
06-11-2025
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu cha Zanzibar.
06-11-2025